NA Richard Mrusha
KAMPUNI ya Wavesleek kupitia Mtandao wao wa Seto waja na suluhisho Kwa wapangaji wa majumbani na hotelini kupitia Huduma ya kiganjani kwa bei nafuu ambapo pia inawapa fursa ya kujitengenezea kipato .
Akizungumza na waandishi Wahabari Mmiliki wa Kampuni ya Wavesleek Hamza Jabir amesema kutokana na kuwepo kwa changamoto wanaopata watu wanaotafuta Makazi pamoja na sehemu za biashara Kampuni hiyo imetambulisha rasimi Huduma hiyo ya Mtandao mpya wa "Seto" ili kusaidia upatikanaji kwa haraka na bila usumbufu wowote.
Mtandao huu unalenga kurahisisha upatikanaji wa Nyumba sehemu za biashara kupitia Mtandao wa Setto Kwa kupakua na kujisajiri na malipo yake ni shilingi elfu 10 tu.
Hata hivyo ameeleza kwamba mwanzo ilikua Ani usumbufu mkubwa Kwa kuwapatia Madalali pesa ya Kodi Kwa mwezi Mmoja hivyo basi kuwepo kwa Mtandao huo utaweza kuleta ahueni kwa wananchi."
AmesemaJabir kuwa Kwa vijana ambao wamekosa Ajira Kwa kupitia Huduma hiyo ya Mtandao huo Seto wataweza kujipatia Ajira Kwa urahisi kama Madalali.
" Nawaomba vijana wachangamkie fursa hiyo ya udalali kupitia Mtandao wa Setto Kwa kusambaza picha za Nyumba ambazo zinapangishwa au kuuzwa, Kwa kufanya hivyo wataweza kupata shilingi elfu 6 kama malipo yao."a
0 Comments