DC BAGAMOYO ATOA MAAGIZO MAZITO FEDHA ZA MIKOPO ZA VIJANA,WANAWAKE NA WATU WENYE ULEMAVU.

 Na Shushu Joel,Chalinze 

MKUU wa wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Mhe Zainabu Issa  ameijia juu  halmashauri ya Chalinze kwa kutokutekeleza kwa haraka agizo la serikali kwa utoaji wa mikopo kwa Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu kwa kusudi la kuyaondoa makundi hayo kwenye changamoto ya kuondokana na umasikini

Mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Zaynabu Issa akifafanua jambo mbele ya madiwani na wakuu wa idara(NA SHUSHU JOEL)

Agizo hilo amelitoa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kwa kumtaka Mkurugenzi wa halmashauri kuhakikisha ifikapo ijumaa anamkabidhi ripoti ya utekwlezaji wa Mikopo ikiwa sambamba na viambatanisho vya benk vikionyesha vikundi vilivyopata fedha. 

Aidha Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa halmashauri  ya Chalinze kumekuwa na mchezo ambao naufuatilia ili kujua kina nani wanafanya jambo hilo la kuonekana pesa za vikundi kuonekana zimeenda kwa wahusika huku wahusika wakidai hawajapata pesa hizo.

"Natoa siku tatu kwa idara ya maendeleo ya jamii kuhakikisha wananiletea idadi ya vikundi vilivyopata pesa za mkopo ikiwa ni kwenye mgawanyo unatakiwa na serikali yaani Wanawake,Vijana na watu wenye Ulemavu pia nahitaja na karatasi za benk zikionyesha pesa zimeingizwa kwenye akaunti zao"Alisema Mkuu wa wilaya  Zaynabu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Hassan Hassan Mwinyikondo amempongeza Mkuu huyo wa wilaya kwa kutambua thamani ya wananchi ambao ndio wapiga kura za Chama cha Mapinduzi. 

Aidha Mwinyikondo amemtaka Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kusitisha zoezi la vikundi kupatiwa fedha za mikopo kupitia halmashauri na badala yake kuzipeleka fedha hizo kwenye kata usika ili wananchi waone jinsi gani serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inavyowajali wananchi wake.


"Endapo pesa hizo zikianza kugawiwa kwenye ofisi zetu za kata zitasaidia wananchi kuweza kurejesha kwa haraka ili na wengine waweze kukopeshwa "Alisema .

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na fedha wa halmashauri hiyo ambaye pia ni Diwani wa kata ya kiwangwa  Marota Kwaga amemwakikishia Mwenyekiti wa halmashauri hiyo kuwa kamati yake imejipanga kuhakikisha inaongeza kiwango cha mapato  kwa kubuni miradi mbalimbali itakayosaidia halmashauri hiyo kupata fedha nyingi ili kuhakikisha ile asilimia kumi ya Mkopo kwa Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu unakuwa kila kijiji.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments