Na Shushu Joel, Chalinze.
MWENYEKITI wa halmashauri ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Ndg Hassan Mwinyikondo amewataka wananchi wa Jimbo hilo kukaa Mkao wa kula kwani sasa ni kipindi cha maendeleo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Chalinze Hassan Mwinyikondo akila kiapo kwa kuikusudiwa yale yanayotendwa |
Hayo ameyasema mara baada ya kula kiapo cha kuwa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo.
Alisema kuwa wananchi wa Chalinze wanahitaji maendeleo na sio kitu kingine hivyo kwa nafasi hii niliyoaminiwa na madiwani wenzangu nitahakikisha kila kata inapata maendeleo sawa kwa kusudi tulilokusudia kwenye Jimbo letu.
"Niwakumbushe watumishi kuwajibika ili kufikia malengo yetu kwa wananchi wetu hivyo uwajibikaji uliotukuka ndio nguzo kubwa ya mafanikio"Alisema Mwinyikondo
Aidha amesisitiza kila mmoja kuweka heshima kwa mwezake ili kuweza kuwa na timu bora ya utendaji.
Naye Juma Mpwimbwi Diwani wa kata ya. Miono amempongeza Mwenyekiti huyo kwa kuweza kupata kura za kishindo na kuweza kuwa kiongozi wa madiwani ndani ya halmashauri hiyo.
Hivyo matumaini yetu makubwa ni kuona maendeleo yanakuja kama ilivyokusudiwa na hili ndilo hitaji la wananchi wa Chalinze.
MWISHO
0 Comments