Na Shushu Joel,Pwani
KUTOKANA na changamoto inayoendelea kutokea nchini kwa baadhi ya sehemu kukosa huduma muhimu ya nishati ya umeme na kupelekea kupungua kwa ufanisi wa baadhi za kazi kwa wananchi mbalimbali ambao wamekuwa wakifanya shughuli zao kwa uhitaji wa umeme.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Chalinze mara baada ya kutembea mradi wa ujenzi wa mradi wa Umeme wa Mwalimu Nyerere(NA SHUSHU JOEL)
Aidha Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amewataka wananchi wa Mkoa huo na Watanzania
kwa ujumla kuendela kuwa na subra kwani serikali ya awamu ya sita chini ya Rais
Samia Suluhu Hassan imejipanga kikwelikweli kwa kusudi la kuhakikisha Tanzania
inakuwa nchi ya pekee Afrika Mashariki kwa uhakika wa upatikanaji wa uhakika wa
Umeme.
“Mpaka sasa
mradi huo wa mwalimu Nyerere unaendelea vizuri katika ujenzi na muda si mwingi
watanzania wataanza kunufaika na mradi huo mkubwa ambao unajengwa kwa fedha za
ndani, hii ni hatua kubwa sana kwa Taifa letu kwa kutumia pesa za ndani
kutekeleza miradi mikubwa ambayo ni faida kubwa kwa watanzania”Alisema Kunenge
Aidha Mkuu
huyo wa Mkoa wa Pwani alisema kuwa kuwepo kwa mradi huo katika Mkoa wa Pwani
umefungua fursa nyingi kwa vijana na wananchi kwa ujumla kwani wananchi
wameweza kunufaika kwa kupata ajira katika nafasi mbalimbali kwenye mradi huo
uligharimu kiasi kikubwa cha fedha.
Aidha Mkuu
huyo wa Mkoa aliongeza kuwa mara baada ya kukamilika kwa mradi huo utaenda
kumaliza kabiza changamoto ya katika katika ya umeme pia Taifa litaingiza fedha
nyingi za kigeni kutokana na uzalisha wa umeme huo kuwa mkubwa kuliko uhitaji
wetu.
Kwa upande wake mmoja wa wananchi ambaye ni mkazi wa Mkoa wa Morogoro Juma Mahina alisema kuwa pindi mradi huo utakapo kamilika utasaidia Taifa letu kwa asilimia mia.
Aliongeza kuwa
mradi wa Mwalimu Nyerere ukikamilika utaenda kujenga ajira nyingi kwa
watanzania kwani umeme ni mtaji mkubwa na huu ni umeme wa uhakikia hivyo
wananchi wanaenda kuwa wenye kipato cha kuridhisha mara baada ya kuanza
kutumika kwa mradi huo.
Aidha Mahina
aliongeza kuwa ni vyema serikali ikawekeza nguvu nyingi za usimamizi ili mradi
huo ukamilika kwa muda ili kuokoa katika katika ya umeme ambao umekuwa
ukijitokeza kwa sababu mbalimbali.
Naye Mariamu
Ally mkazi wa Simiyu mara baada ya kuzungumza na Mwandishi wa Habari wa HABARI
MPYA BLOG alisema kuwa wao wanausubili mradi huo kwa hamu kwani ni mkombozi
wetu.
Aidha
aliongeza kuwa pongezi ziende kwa serikali ya Mkoa wa Pwani chini ya Abubakar
Kunenge ambaye amekuwa mstali wa mbele kama Mkoa kuhakikisha mradi huo
unakamilika kwa haraka ili kusaidia Taifa kwenye Nyanja ya Nishati.
“Awamu ya
sita ni serikali sikivu na yenye uchu ya kuona wananchi wake wanapata miradi
mikubwa kwa fedha za ndani hivyo Rais Samia Suluhu HJassani ni jembe letu
tunalolitegemea kutuvusha hapa tulipo “
MWISHO
0 Comments