Na Shushu Joel, Kibaha
MWENYEKITI wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Pwani Jackson Kituka amewakumbusha viongozi wa jumuiya hiyo katika wilaya ya Kibaha kuhakikisha wanaacha alama katika nyadhifa zao za uongozi kwa wananchi wanaowaongoza.
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Pwani Jackson Kituka akiteta jambo na mmoja wa viongozi wa jumuiya hiyo wilaya ya Kibaha mara baada ya kikao maalum(NA SHUSHU JOEL)
Hayo
ameyasema alipokuwa akizungumza na viongozi wa jumuiya hiyo katika wilaya ya
Kibaha ambapo amewasisitiza kuwa kiongozi bora ni Yule anayesimamia miongozo
kwa ajili ya kuisaidia jamii anayoiongoza
“Wengi
tumekuwa na mawazo tofauti juu ya uongozi hivyo nawaombeni viongozi wezangu
tuweze kujitolea kwa dhati kwa wananchi wetu ili kuweza kuweka alama kwa
wananchi wetu”Alisema Kituka
Aidha Mwenyekiti huyo aliwakumbusha viongozi wa jumuiya hiyo kuwa wazazi ndio nguzo kubwa katika jumuiya zote za chama cha mapinduzi hivyo ni lazima kila kiongozi kuonyesha ukomavu wake ili jumuiya zingine ziweze kujifunza kupitia wazazi.
“Rais wetu
amekuwa akitenda mambo mengi mema kwa jamii na hasa yale ya kimaendeleo kwa
watanzania hivyo ni muhimu sie kama wazazi kuhakikisha tunakuwa mstali wa mbele
kwenye kubeba yale yote yanayofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan”Alisema
Mwenyekiti huyo wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Pwani.
Aidha
aliongeza kuwa matamanio yangu ni kuona kila kiongozi wa jumuiya ya wazazi
kuanzia ngazi ya shina mpaka kata anakuwa kiongozi wa kuigwa kwa kuweka alama
za uongozi kwa jamii.
Mwajuma
Mohamed amempongeza Mwenyekiti huyo kwa juhudi zake anazozifanya kwa wana chama
kwa kusudi la kuwaweka pamoja na kuwakumbusha wajibu wao kila mmoja wetu.
Aliongeza
kuwa kiongozi unapoweka alama ya uongozi unakuwa ni mfano mkubwa kwa jamii
hivyo maneno ya Mwenyekiti ni ya kuigwa kwa viongozi wote.
MWISHO
0 Comments