RC KUNENGE AUTAFUNA MFUPA ULIOSHINDIKANA.

 Na Shushu Joel,Pwani

WANANCHI wa Mkoa wa Pwani wamempongeza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge kwa kufanikisha kutafuna mifupa iliyowashinda wengi.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akifafanua jambo

Juma Ally (63) mkazi wa miono alisema kuwa Mkuu wa Mkoa amekuwa kiongozi wa pekee katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo ndani ya mkoa wetu.


Aidha Ally alisema kuwa Mkuu wa Mkoa Kunenge amekuwa akipamban sana migogoro ya Ardhi katika maeneo mbalimbali kwa kusudi la kuongeza wawekezaji kutokana na uwepo material mengi pia amewataka viongozi kuweza kujifunza ili kuendana kwa pamoja.


"Pwani ilikuwa na changamoto lukuki lakini tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kumleta Mkuu wa Mkoa Kunenge mambo mengi yamekuwa yakienda kama tunavyohitaji wananchi hivyo Mkuu wetu wa Mkoa ni kiongozi wa kuigwa" Alisema Ally.


Naye Bi, Fatuma Mohamed amemsifi Mkuu wa Mkoa kwa jinsi ambavyo amekuwa mbinifu wa kuwaleta watu karibu kwa kufanya matamasha mbalimbali ikiwemo ya Biashara, michezo kwa kusudi la kutengeneza mahusiano yaliyo bora baina ya wawekezaji na wananchi.


Aliongeza kuwa Pwani kwa sasa ina viwanda vingi vikubwa kwa vidogo na imefanikiwa kutengeneza ajira nyingi kwa watu wengi wa Pwani.


Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akizungumza kwa njia simu alisema kuwa yeye awezi kusema sana bali wananchi wanaona kile kinachofanyika.


Aidha aliongeza kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inahitaji kuwasogezea wananchi miradi ya maendeleo zaidi .


" Sie kama Pwani tunashirikiana sana ili kuwapatia wananchi maendeleo zaidi" Alisema Kunenge.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments