Na Shushu Joel, Kibaha.
MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amesema kuwa Pwani wamejipanga kuonya ni jinsi gani wamedhamilia kufanya mambo makubwa na ya kushangaza katika tamasha la tatu la uwekezaji na biashara.
![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari(NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza na HABARI MPYA BLOG Rc Kunenge alisema kuwa Mkoa wa Pwani ni miongoni mwa Mikoa iliyojaa fursa kwa ajili ya wawekezaji wa aina mbalimbali hivyo siku tano za maonyesho zitaenda kujieleza.
"Pwani tuna viwanda vingi vikubwa kwa vidogo ambavyo asilimia kubwa vimewekeza kwenye kipindi cha awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na wote hao watashiriki na wataonyesha kile wanachokizalisha" Alisema Kunenge.
Aidha aliongeza kuwa tumefungua fursa kwa wananchi wote wa Mkoa wetu kuweza kushiriki kwa kuuza bidhaa zao ili waweze kujipatia kipato kupitia maonyesho hayo ya pekee hapa nchini .
Pia alisema kuwa maonyesho hayo yanaenda Sambamba na ufunguaji wa milango kwa wawekezaji kuweza kuwekeza hapa Pwani kwani mali ghafi zipo za kutosha na serikali imekuwa ikiwahitaji sana wawekezaji.
Kwa upande wake Juma Malimi ambaye ni mmoja wa wananchi wanaojishughulisha na biashara ya uuzaji wa viwanja amesema kuwa Mkuu wa Mkoa Abubakari Kunenge ni kiongozi mwenye maono ya mbali kwa wawanchi wake kwani ubunifu huu unaenda kufungua fursa kwa wananchi wengi.
Aidha aliongeza kuwa uwepo wa maonyesho ya tatu ya uwekezaji na Biashara wananchi wa Pwani tunaenda kuwa na kipato cha kutosha kwani ongezeko la viwanda linaenda kuongezeka na Biashara nyingi zinaenda kukua.
"Tunampongeza sana Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumleta Kunenge katika Mkoa wetu kwani ubunifu wake ni wa hali ya juu huku kusudi Lake kubwa ni kuwaona wananchi wananeemeka na Ardhi yao ya Pwani.
Naye Fatuma Ally ni mfanyabiashara wa chakula maarufu Mama Ntilie amempongeza Mkuu wa Mkoa kwa namna ambavyo amewatengenezea fursa Mama Ntilie kwani tutafanya biashara kwa kiwango cha juu kutokana na uwepo wa maonyesho ya tatu ya uwekezaji na Biashara ambayo yanatarajiwa kuanza tarehe 5 mpaka 10.
MWISHO

0 Comments