Na Shushu Joel,Pwani
MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amepiga marufuku uvamizi na uvunaji holela wa miti kwenye maeneo ya vijiji,vyanzo vya maji na misitu ya hifadhi kwani kuna watu wamevamia kwenye hifadhi na kufanya uharibifu mkubwa kwenye misitu kitu ambacho kinapelekea kutishia uendelevu wa hifadhi ya mazingira na vyanzo vya maji.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge akisisitiza jambo(NA SHUSHU JOEL)
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake Kunenge alisema kuwa tabia hizo za ukataji
wa miti ovyo kumepelekea kuwepo kwa changamoto nyingi za kitabia ya nchi hivyo
niwatake wale wote wanaojishughulisha na kazi hizo kuacha mara moja.
“Sheria ya
misitu Na 14 sura ya 323 iliyorejeshwa mwaka 2022,taratibu na kanuni za misitu
za mwaka 2004 tangazo la serikali (GN) Na 417 la mwaka 2019, Na 59 la mwaka
2022 na mwongozo wa uvunaji endelevu na biashara ya mazao ya misitu wa mwaka
2017 vinaelekeza uvunaji wa mazao ya misitu” Alisema Mkuu wa Mkoa.
Aidha
alisema kuwa ni vyema sasa wale wote wanaoendeleza uvunaji holela katika maeneo
ya misitu katika Mkoa wa Pwani wahakikishe wanaacha mara moja tabia hiyo kwa
kusudi la kulinda misitu.
Mbali na
agizo hilo Mkuu wa Mkoa huyo amewataka waandishi wa habari wa Mkoa huo
kuhakikisha wanatumia kalamu zao kufikisha ujumbe kwa jamii ambazo zimekuwa na
tabia ya kuvamia misitu holela.
MWISHO
0 Comments