Na Shushu Joel,Pwani.
WAANDISHI wa habari Mkoa wa Pwani wamepewa elimu juu ya umuhimu wa kuelimisha jamii jinsi ya kujikinga na maambukiza ya ugonjwa wa COVID 19

Waandishi wa habari wa Mkoa wa Pwani wakijengewa uwezo juu ya masuala ya kuandika hbari za COVID 19 na aliyesimama ni Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dr. Gunini Kamba(SHUSHU JOEL)
Akitoa elimu
hiyo kwa waandishi wa habari wa Mkoa huo Dr, Caroline Akim kutokea WHO alisema kuwa waandishi ni jeshi kubwa lenye
uwezo wa kufikisha taarifa za haraka kwa umma hivyo ni jambo la muhimu sana
kuwaelimisha waandishi kwa kusudi la kuisaidia jamii.
Aidha
aliongeza kuwa ugonjwa huu umekuwa na changamoto kubwa kwa jamii lakini
kutokana na juhudi mbali mbali ambazo zimekuwa zikichukuliwa na serikali
mapambano yamekuwa ni makubwa ili kuwasaidia wananchi wa Taifa husika.
“Ugunduzi wa chanjo umekuwa ni msaada mkubwa kwa watu ndio maana hata miaka ya nyuma palipogundulika chanjo ilifanikiwa kuzuia chanjo kwa watoto na ndio maana hata ujio wa chanjo ya COVID 19 imeleta matokea chanya kwa jamii hivyo chanjo ni muhimu sana na jamii husika iendelee kupata chanjo ili kuondokana na magonjwa kama hayo” Alisema Dr Akim
Pia alisema
kuwa chanjo zote zilizopo nchini ni salama na zina faida kubwa kwa wananchi
hivyo zoezi hili la kupata chanjo liendelee ili kuepuka usumbufu pindi mtu
anapoambukizwa ugonjwa huo.
Aliongeza
kuwa lengo kubwa la kuanzishwa kwa chanjo hiyo ni kwa ajili ya kuwakinga wananchi
dhidi ya ugonjwa huo wa Covid 19 hivyo kusudi ni kuhakikisha watanzania wote
wanapata chanjo ili kuepukana na maambukizi ya ugonjwa huo.
“ Tuwaombe
waandishi wa habari kuhakikisha wanatumia kalamu zao vyema kwa kusudi la
kuisaidia jamii juu ya umuhimu wa upataji wa chanjo”Alisema Dr Akim
Aidha
aliongeza kuwa mpaka sasa takwimu za ugonjwa wa COVID 19 zinaonyesha kuwa watanzania waliopata ugonjwa huo ni 38,205
na vifo mpaka sasa ni watu 845.
Kwa upande
wake mmoja wa waandishi wa habariwalioshiriki katika semina hiyo Gustaph Haule
ameipongeza WHO kwa kutambua
umuhimu wa waandishi wa habari katika jukumu la kuielimisha jamii kupitia vyombo mbali mbali vya habari.
Aidha alisema kuwa waandishi wako tayari
kuisaidia serikali katika suala zima la utoaji elimu kupitia taaluma zao.
Pia
amewataka waandishi kuhakikisha wanayatumia mafunzo ya COVID 19 kama chachu ya
usambazaji wa elimu kwa jamii ili waweze kupata chanjo na kujiongezea kinga
katika miili yao.
MWISHO
0 Comments