Na Shushu Joel, Dar
![]() |
Naibu Waziri wa Ardhi akisisitiza jambo mbele ya warasimishaji wa Ardhi |
NAIBU Waziri
wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Ridhiwani Kikwete amewakumbusha wananchi
kuhakikisha wanachukua Hati miliki za maeneo yao ili ziweze kuwasaidia katika
mambo mbalimbali ikiwemo hata kukopesheka kwa ajili ya kukuza biashara zao.
Rai hiyo
ameitoa alipokuwa kwenye mkutano na makampuni yanayofanya kazi y urasimishaji
katika Mkoa wa Dar es Salaam.
“Mwananchi
unapokuwa na hatimiliki yako inakuwezesha kuwa na faida kubwa sana na eneo lako
kutokana na kuwa na hati zako hivyo inakufanya kukopesheka kwenye taasisi
mbalimbali za kifedha kitu ambacho kitapelekea kuinua uchumi wako” Alisema
Kikwete.
Aidha kikao
hicho kimeudhuliwa na kamishina msaidizi Mkoa wa Dar es Salaam Shukrani Kyando.
MWISHO
0 Comments