LIONS CLUB YAWAKOSHA WANANCHI CHALINZE


Baadhi ya wananchi wa Msoga wakipatiwa huduma za kiafya na wataalu kutoka Lions Club

Na Mwandishi wetu

 Wanachama wa Lions Club ya Dar Mzizima wametoa matibabu ya Macho, Kupima presha na sukari kwa wananchi 2000 katika halmashaur ya Chalinze wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani


Wakizungumza na waandishi wa Habari walisema kuwa lengo ni kutoa msaada kwa jamii ili kuweza kutambua thamani ya mtu kuwa na Afya bora.


Wanachama hao waliendesha kambi ya siku nne  katika Hosptali ya Msoga Chalinze kwa ajili ya kuhudumia wananchi wenye matatizo mbalimbali ya kiafya.ambao wote walifanikiwa kupatiwa vipimo na ushauri wa kitaalamu zaidi kutoka kwa madktali bingwa .


Kwa kushirikiana na Lions Club ya Dsm  Infinity   pia walitoa zawadi mbalimbali kwa ajili ya  wakina mama waliojifungua,  na wajawazito  walioko katika hosptali hiyo sambamba na kutoa taulo za kike kwa wasichana 70

Mbali na matibabu hayo Club hiyo pia ilitoa chakula kwa kusudi la kusaidia huduma hiyo ili pale unapokuja kupata huduma hiyo basi unakula pale pale.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments