MIKATABA YA USIMAMIZI WA LISHE KWA WATOTO MASHULENI WASAINIWA

Julieth Ngarabali. Pwani

 Mkuuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amewasainisha mikataba  ya usimamizi wa lishe wakuu wa Wilaya zote ndani ya mkoa huo ambapo watapaswa kusimamia utekelezaji huo kwa kipindi cha miaka 8.

Wanafunzi wa darasa la awali shule ya St. Joseph day care centre  Kibaha wakipata uji  (lishe) shuleni hapo.

Mkataba huo unasainiwa huku hali ya lishe kwa kipindi cha  2022 kuna asilimia 23.3 ya watoto wenye udumavu, takwimu ambazo ni kwa mujibu wa Ofisa lishe mkoani humo Pamela Meena


Akizungumza baada ya kutiliana saini  mikataba hiyo Kunenge amesema mikataba hiyo ina viashiria 14 vya utekelezaji kutoka 10 vya awali.


"Mkataba huu una viashilia 14 vya utekelezaji ambavyo watendaji wanapaswa kuvisimamia ikiwemo kutenga pesa kiasi cha sh 1000 (elfu moja)  kwa kila mtoto mwenye umri wa miaka mitano Ili zitumike kwa lishe maeneo ya shuleni "amesema.


Vingine ni asilimia ya sampuli za chumvi kutoka kwenye kaya zilizokusanywa kupitia wanafunzi na kupimwa uwepo wa madini joto.


Amesema matokeo ya kazi hizo yatapimwa kwa vitendo kwenye kila shule ili kuona kama yaliyomo kwenye mkataba yanatekelezwa ama la na ikionekana kuna kinyume  hata sita kuchukua hatua kwa watendaji  kulingana na kanuni zilizopo.


Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani  Dokta ,Gunini Kamba amesema hali ya lishe ndani ya mkoa huo imeendelea kuimalika ikilinganisha na miaka ya nyuma jambo ambalo limetokana na juhudi za wataalamu wa lishe kutoa elimu kwa jamii..


"Baadhi ya wazazi walikuwa na mwamko mdogo juu ya lishe bora wakiamini kuwa vyakula kama chipsi mayai ndio lishe bora jambo ambalo siyo bali hata mbogamboga pia ziko kwenye kundi la lishe"amesema Dkt. Kamba


Amesema mikakati yao baada ya kusaini Mkataba huo ni kupunguza idadi ya vifo  vya watoto wachanga 11 kati ya vizazi hai1000 ambavyo vilikuwepo kwenye ripoti ya mwaka jana.


Mmoja wa wazazi Adela Piniel amesema elimu zaidi kuhusu umuhimu wa lishe bora itolewe kwa walezi na wazazi ili waone umuhimu wa watoto kupata lishe ya kutosha hasa kwenye umri wa miaka 0 hadi miaka nane (8 )  kwani ni fursa pekee ya kumjenga mtoto  kwa ujenzi wa Taifa letu. 


Mwisho

Post a Comment

0 Comments