MAKAMU WA RAIS UFUNGUZI KONGAMANO LA MAZINGIRA IRINGA

 Na Shushu Joel

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Philip Mpango akihutubia waandishi na wahariri juu y a umuhimu wa utunzaji vyanzo vya maji.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa

Dkt.Philip Mpango amewataka baadhi ya viongozi wanaochangia katika

uharibifu wa mazingira na vyanzo vya maji kuacha mara moja ili kunusuru

Taifa dhidi ya athari za uharibifu zinazojitokeza hivi sasa.

Makamu wa Rais amesema hayo  wakatiakifungua Kongamano la Wahariri na Wadau wa Uhifadhi Mazingira naUtunzaji wa Vyanzo vya Maji linalofanyika katika Ukumbi wa Masiti mkoaniIringa. Amesema ni vema viongozi kuachana na maslahi binafsi ili kunusuru

mito yote kwani madhara kwa jamii ya watanzania ni makubwa zaidi.

Makamu wa Rais amesema ni lazima kushirikiana na kuwa na jitihada za

pamoja baina ya serikali, dini, sekta binafsi, vyombo vya Habari pamoja na

vyama vya siasa katika kupambana na uharibifu wa Mazingira nchini.

Halikadhalika Makamu wa Rais amewaasa Waandishi wa Habari kuendelea

kutumia ushawishi walionao katika jamii kuihamasisha jamii kuhusu utunzaji

wa mazingira na kuziagiza taasisi za Serikali kuhakikisha zinawashirikisha

Waandishi wa Habari na Vyama mbalimbali vya Wanahabari vinavyojitoa

kushirikiana na Serikali katika kukabiliana na athari za uharibifu wa mazingira.

Pia amewasihi wahariri na waandishi kuandika habari na taarifa za kuelimisha

umma za kiuchunguzi na kuepukana na kuandika habari bila kufanya tafiti za

kutosha au kujiridhisha hivyo kupelekea habari za upotoshaji hapa nchini.


Makamu wa Rais amewaasa wahariri na wanahabari wote kwa ujumla kuwa

wazalendo na kulinda taswira na maslahi ya nchi kwa kuepuka kuwa mstari

wa mbele katika kutetea mambo yanayohujumu taifa. Amewataka kujiepusha

na kupokea fedha, mali au vishawishi vingine kutoka kwa watu wachache

wenye jeuri ya pesa au madaraka ili kupindisha ukweli wa mambo kinyume

na maslahi ya taifa au wananchi wengi wanyonge wasio na sauti.

Pia ametoa wito kwa wanahabari wito kusaidia kuelimisha jamii kuhusu fursa

zitokanazo na utunzaji wa mazingira ikiwemo biashara ya Kaboni, inayofanyika

kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi duniani hususan, kwa kupunguza

gesijoto. Amesema biashara hiyo ni fursa ambayo itachangia katika pato la

Taifa na kuimarisha suala zima la uhifadhi wa mazingira.

Makamu wa Rais amewasihi kutumia Kongamano hilo kufanya mijadala ya

kina ya kujenga na kupata maazimio ambayo pamoja na mambo mengine,

yatajumuisha hatua mbalimbali zitakazochukuliwa katika kuongeza juhudi za

kuhabarisha umma kuhusu utunzaji na ulinzi wa mazingira hususan katika

Vyanzo vya Maji.


Kwa upande wake mwenyekiti wa Kituo cha Wanahabari Watetezi wa

Rasilimali na Taarifa (MECIRA) amesema wanahabari watetezi wa rasilimali

kwa umoja wao watahakikisha wanashiriki katika mapambano ya kuhakikisha

wanalinda na kuhifadhi na kutetea rasilimali za nchi ikiwemo suala la

mazingira. Aidha ametoa wito kwa mamlaka za usimamizi kuwasimamia

watendaji waliopewa dhamana ya ulinzi wa vyanzo vya maji ili waweze

kutimiza wajibu wao na kuepukana na athari za uharibifu zinazojitokeza hivi

sasa.

Wanahabari hao watetezi wa Rasilimali wamesema wameshuhudia mto Ruaha

ukifikisha siku 130 bila kutiririsha maji licha ya maji hayo kuwepo katika

chanzo cha mto ambao huzuiliwa na baadhi ya wananchi wachache

wanaofanya shughuli mbalimbali za kilimo jirani na mto huo.

Kongamano hilo linaratibiwa na Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali

na Taarifa (MECIRA) kwa kushirikiana na Jukwaa la Wahariri nchini na

linashirikisha wanahabari, wadau wa mazingira, viongozi wa serikali, dini,

vyama vya siasa pamoja na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments