Na Shushu Joel, Rufiji
WANAWAKE wa Mkoa wa Pwani wameambiana kutembea kifua mbele kwa kipindi hiki kutokana na kile walichokifanya katika uchanguzi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) mara baada ya kumpigia kura za kishindo na kumchagua Mariam Ulega kuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (Mbaraza) kutokana na kile ambacho ameanza kuwaonyeshea wanawake wa Mkoa huo.

Mariam Ulega akiwa katika moja ya heka heka heka zake(NA SHUSHU JOEL)
Rai hiyo
imetolewa na baadhi ya wanawake wa Mkoa huo kwa kusema kuwa sababu ya mambo ambayo yamekuwa
yakifanywa na kiongozi huyo ya kuwasaidia wanawake wa Mkoa huo ili waweze
kuondokana na baadhi ya changamoto mbalimbali ambazo zilikuwa zikiwakabili
wanawake wa Pwani.
Fatma
Mapanga ni mkazi wa wilaya ya Bagamoyo alisema kuwa Mbaraza wetu Mariam Ulega ni
kiongozi mwenye uchungu mkubwa na jumuiya yetu ndio maana amekuwa akikutana na wanawake wa Mkoa wa
Pwani mara kwa mara na kuwapatia mafunzo ya kila namna ili mradi tu aweze kuwainua kiuchumi wanawake wa maeneo mbalimbali katika Mkoa wa
Pwani.
Aidha
alisema kuwa wanawake tunatakiwa kuiga yale yanayofanywa na Maria Ulega
kutokana na kile ambacho amekuwa akikihakikisha kinawafanikishia wanawake
katika kukuza uchumi wao wa kila siku ili waweze kuondokana ana matatizo ya
kuwategemea waume zao.
“Kwa kweli
kipindi hiki tumefanikiwa kupata kiongozi ambaye tuna matumaini naye makubwa
kuwa anaweza kutuvusha na kufika mbali sana kutokana na kiu yake ya kuwaona
wanawake wenzake wana kuwa na uchumi wa kujitegemea na kuondokana na utegemezi
kutoka kwa wanaume” Alisema Bi. Fatma
Kwa upande
wake Mariyam Masaninga amempongeza Mbaraza Mariam Ulega kwa jinsi ambavyo
amekuwa akijitoa maisha yake ili kuwasaidia wanawake wa Pwani waweze kuinuka na
kuachana na tabia ya kuwa tegemezi kwa wanaume.
Aidha aliongeza
kuwa uimara wa Mjumbe huyo wa Mkutano Mkuu wa UWT ni kutokana na kiu kubwa
aliyonayo ya kuhitaji wanawake wote wasonge mbele kiuchumi .
Akizungumza
kwa njia ya simu Mjumbe huyo mara baada ya kupigiwa simu alisema lengo ni
kuhakikisha wanawake Mkoa wa Pwani wanakuwa kiuchumi kwa lengo la wao.
Aidha
amewapongeza wanawake kwa ushirikiano waliompatia tangu apate nafasi hiyo ya
ujumbe kwani peke yake ni sawa na bure hivyo kwa umoja huo tunaweza kufika
mbali katika kumsaidia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan
MWISHO
0 Comments