RAIS DKT SAMIA NI ZAO LA BIBI TITI: MGALU

 Na Shushu Joel, Rufiji

MBUNGE wa viti maalum  Mkoa wa Pwani Bi Subira Mgalu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo amekuwa akitenda kazi zake kwa watanzania.

Mbunge wa Viti Maalum Subira Mgalu akiteta jambo na Mbaraza Mariam Ulega{NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya kumuenzi Hayati Bibi Titi  Mohamed  Mgalu alisema kuwa Rais Dkt Samia amemtendea haki  Bibi  Titi kwa ufanyaji kazi.


" Kama leo hii Hayati Bibi Titi angekuwa hai angejionea  uthubutu mkubwa unaofanywa na Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan katika uletaji wa maendeleo kwa wananchi" Alisema Mgalu.


Aidha Mhe Mgalu amesisitiza kuwa Hayati  Bibi Titi Mohamed anatakiwa kuenziwa kwa vitendo ili historia yake iendelee kudumu vizazi na vizazi.

Naye Scolastica Ally amesema kuwa kizazi za enzi hizo kilifaidi sana kwa jinsi ambavyo Hayati Bibi  Titi Mohamed alivyokuwa akiwashauri Wanawake wenzake.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments