Na Shushu Joel, Rufiji.
MWENYEKITI wa Jumiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania Mkoa wa Pwani Bi Zaynabu Vulu ameitaka Wizara ya Sanaa,Michezo na Utamaduni kuweza kuanzisha Taasisi ya kumbukumbu ya Bibi Titi Mohamed kama ilivyo kwa taasisi zingine za wasisi wa Taifa letu kama vule taasisi ya Mwalimu Nyerere.
Aidha alisema kuwa ni vyema sasa maadhimisho ya kumbukumbu ya Bibi Titi Mohamed yakafanyika katika Mikoa mbalimbali kwa kusudi la kuijua historia yake ya Hayati Bibi Titi.
Kwa upande wake Mariam Ulega ambaye ni mbaraza kutokea Mkoa wa Pwani amewapongeza wote walioshiriki katika maadhimisho hayo ya kumuenzi Hayati Bibi Titi Mohamed pia wamejua historia ya mwasisi huyo wa UWT Taifa.
Aidha amewataka wanawake wote nchini kufuata mienendo ya Hayati Bibi Titi Mohamed. kama alivyokuwa akiitendea haki jumuiya hiyo.
MWISHO
0 Comments