Na Shushu Joel
![]() |
| Katibu wa Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mkoa wa Pwani akisisitiza jambo mbele ya wananchi wa kata ya njia nne.(NA SHUSHU JOEL) |
TAASISI ya
kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Mkoani Pwani imetembelea wilaya ya Mkuranga
katika kata ya Njia nne kijiji cha Miteza ili kujionea alama iliachwa na Hayati
Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere kwa lengo la kujifunza na kutanzama
jinsi gani kiongozi huyo alivyokuwa na maono ya mbali katika Taifa hili.
Akizungumza mara baada ya kuzuru katika moja ya darasa lililojengwa na mhasisi huyo wa Taifa hili katibu wa Taasisi hiyo Omary Pumzi alisema kuwa Hayati Baba wa Taifa alikuwa akipambana kwa vitendo na maadui watatu ambao ni Ujinga,Elimu na maradhi na ndio alikuwa akifika kwenye maeneo ambayo yanakuwa na maswali mengi ya kujiuliza kwa kipindi hicho alifikaje.

Moja ya majengo ya shule yaliyojengwa na Hayati Baba wa Taifa Mwl Nyerere
Aidha
alisema kuwa ni vyema viongozi wakafuata nyayo za mhasisi huyo wa Taifa kwa
makusudi ya kusaidia wananchi.
Naye Diwani
wa kata hiyo Ally Mbwera ameipongeza
Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kwa kutambua thamani ya mhasisi wa
taifa letu na kutembelea kwenye kata yake ili kujionea kile kilichofanywa na
Hayati Baba wa Taifa.
MWISHO

0 Comments