WAANDISHI WA HABARI PWANI WAPIGWA MSASA SHULE BORA.

Na Shushu Joel, Pwani.

WAANDISHI wa Habari kutoka katika  vyombo mbalimbali katika Mkoa wa Pwani leo wamenolewa namna ya kuandika habari za Shule Bora zilizopo kwenye maeneo yanayowazunguka kwa kusudi la jamii kutambua kile kinachofanywa na Serikali ya awamu ya sita.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Zuwena Omary akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari katika warsha ya Shule Bora(NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza na Waandishi hao wa Habari Katibu Tawala wa Mkoa huo Zuwena Omary alisema kuwa Serikali inamakusudi makubwa sana na Waandishi wa Habari katika kuwatumia ili waweze kuandika habari zenye uhakika za uwepo wa Shule Bora katika Mkoa na ndio maana imeamua kuwapatia mafunzo hayo  maalumu huku lengo likiwa  kuwawezesha   kuandika habari hizo.


Aidha Katibu Tawala huyo amewakumbusha maafisa habari wa serikali kuhakikisha wanakuwa na umoja na ushirikiano na wanahabari kwani kwa kupitia wanahabari  na Taasisi husika watatengeneza umoja wenye tija na manufaa makubwa kwa nchi.

Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mjadala wa warsha wa Shule Bora.

 Khadija Kalili  kutoka Michuzi Blog ni mmoja kati ya  Waandishi wa Habari kwenye mafunzo hayo  amesifu uwepo wa mafunzo hayo na kusema kuwa endapo wana habari wakithaminiwa na kupewa fursa kwenye mafunzo mbalimbali mambo mengi yataonekana kwa jamii kwa kutangazwa na vyombo mbalimbali vya habari,

MWISHO

Post a Comment

0 Comments