Na Shushu Joel.
![]() |
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Pwani Mariam Ulega akifurahia jambo na baadhi ya kina Mama hawapo pichani(NA SHUSHU JOEL) |
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Pwani Bi Mariam Ulega ameikumbusha jamii kuendelea kujitolea kwa hali na mali ili kuwasaidia watoto wasio jiweza na wale walio kwenye mazingira magumu( Yatima) ili nao wajisikie kama wapo na wazazi wao.
Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na Wananchi mbalimbali alipokuwa akitimiza moja ya majukumu yake ya kuhamisisha wanawake kujiunga kwenye jukwaa hilo.
"Hata wao hawakupenda kuwa yatima na kuishi kwenye mazingira magumu walitamani kuwa na wazazi wao kama ilivyo kwa watoto wengine lakini mapenzi ya Mungu hayazuiliki hivyo tuendelee kuwapenda na kuwahudumia pindi tunapopata nafasi ya kufanya hivyo" Alisema Mwenyekiti huyo Mariam Ulega.
Aidha alisema kuwa Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Pwani linaandaa namna ya kuwasaidia watoto hao angalau 10 kwa kusudi la kuwashika mkono katika masuala ya shule ili kuwasaidia kupata elimu itakayowasaidia baadae katika maisha yao.
Naye Fatma Haji amempongeza Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Pwani Bi Mariam Ulega kwa jinsi ambavyo amekuwa msaada mkubwa kwa jamii katika masuala mbalimbali.
Aidha amemtaka kuendelea na moyo huo wa kujitoa kwa jamii kwani kuna siku Mungu atanlipa.
MWISHO
0 Comments