NA SHUSHU JOEL
![]() |
Kmanda wa jeshi la polis Mkoa wa Pwani ACP, Pius Lutumo akizungumza mbele ya waandishi wa habari. |
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia madereva 17 wa magari yanayosafirishwa kutoka Bandari ya Dar Es Salaam kwenda nje ya nchi(IT)kwa kosa la kusafirisha abiria kinyume cha sheria ya usalama barabarani sura ya 168 inayokataza magari hayo kusafirisha abiria.
Magari hayo ya IT yanayoanzia safari zao Bandari ya Dar es salaam kwenda nchi za Zambia, Rwanda, Burundi na Kongo kupita mikoa ya Pwani, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Geita na Kagera yamekuwa yakisababisha ajali na kuleta madhara makubwa kwa abiria, hivyo hii ni operesheni endelevu ili kuzuia biashara hiyo hatarishi.
Wito wa Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani ni kuwataka abiria kutumia usafiri rasmi wa umma ili kuepusha usumbufu wanaoweza kuupata safarini kwa kukosa haki zao za msingi inapotokea ajali watumiapo magari ya IT. Aidha madereva wanaoendelea kukaidi na kuvunja sheria ya usalama barabarani kwa makusudi wataendelea kukamatwa na kufikishwa mahakamani.
0 Comments