Na Shushu Joel,Temeke.
JUMUIYA ya Wazazi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika wilaya ya Temeke Mkoa wa Dar es Salaam imewataka wanachama wa Jumuiya hiyo kuhakikisha wanajiunga na umoja wa Sacos ili kuweza kujipatia nafasi ya kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza
na viongozi wa Jumuiya hiyo kuanzia ngazi za matawi mpaka ngazi za wilaya
Mwenyekiti wa kamati ya utekelezaji wa
wilaya hiyo Bi, Husna Madenge alisema kuwa unapojiunga kwenye Sacos hiyo
kuna manufaa makubwa kama mwanachama utayapata kutokana na kile kinachozalisha
na Sacos hiyo.
“Kina Mama
mnazijua chanagmoto tunazozipata kwenye mikopo ya watu binafsi hivyo ujio wa
Sacos yetu ya wazazi ni suluhisho la matatizo yetu” Alisema Bi,Madenge.
Aidha
amewataka wana jumuiya hiyo kuweza kuendelea kumiminika na kujiunga kwenye
umoja huo ili ongezeko lizidi kuwa kubwa na mikopo iweze kutoka kwa wanachama
kwa haraka kama ilivyokusudiwa na jumuiya hiyo ya wazazi katika wilaya ya Temeke.
Naye Juma Keya ambaye ni katibu wa Jumuiya ya Wazazi Tawi la Yasemwayo lilipo kata ya Tuangoma katika wilaya ya Temeke amempongeza Mwenyekiti huyo kwa kuja na wazo hilo lenye kuleta maendeleo kwa Jumuiya ya Wazazi.
Pia
amewataka wana Jumuiya wa Tuangoma kujiunga na Sacos hiyo ili kuweza kujikwamua
kiuchumi na kuweza kusimama imara na kujiongezea kipato kwa ajili ya maendeleo.
MWISHO
0 Comments