Na Shushu Joel
| Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Temeke Khamis Islam akifuatilia jamabo kwa makini |
MWENYEKITI wa
Jumuiya ya Wazazi kutokea Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Temeke Mkoa wa
Dar es Salaam Khamis Islim amewakumbusha Wazazi umuhimu wa malezi bora na yenye
msingi kwa watoto ili kuwasaidia watoto wetu kuweza kuwa na maadili mema kama
waliyoyapata wao kipindi hicho.
Rai hiyo
ameitoa alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa Jumuiya hiyo katika
moja ya vikao vyake anavyoendelea kuvifanya katika wilaya hiyo.
Aidha
Mwenyekiti huyo alisema kuwa Wazazi wengi wamekuwa wakiiachia serikali sana
malezi ya watoto wao bila wao kujihusisha na chochote kitu ambacho kinapelekea
kukosekana kwa maadili mema ambayo sie enzi zetu tuliyapata.
“Vijana wetu
wamekuwa na tabia za ajabu sana kile ambacho akikubaliki katika jamii” Alisema
Islim
Pia alisema kuwa ni muhimu kutambua malezi bora yanaanza na wewe, Hivyo kama wazazi tunapaswa kusaidiana katika malezi sio mtoto wa jirani anapofanya kosa unamsubilia mzazi wake wakati na wewe ni mzazi na unapaswa kuonya kile kilichofanywa na motto huyo
Naye Ivonne
Tibanywana ambaye ni mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi wilaya
akiwakilisha vijana kutokea wazazi amempongeza Mwenyekiti huyo kwa kutambua
kuporomoka kwa malezi mema kwa vijana wa kisasa hivyo yeye kama mwakilishi wa
kundi hilo atahakikisha ujumbe huo unawafikia vijana kila kukicha.
Aidha
amemuomba mwenyekiti huyo wa wazazi kuendelea kupaza sauti ili kuhakikisha
jambo hilo la maadili kwa vijana linarudi kwenye nafasi yake.
MWISHIO
0 Comments