Na Shushu Joel, Dar.
MWENYEKITI wa Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Pwani Bi Mariam Ulega amezidua Taasisi ya CHAWA wa MAMA kitaifa katika Mkoa wa Dar es Salaam katika ukumbi wa karinjee ambapo malengo ya Taasisi hiyo ni kuyasema mazuri yanayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.
![]() |
| Bi, Mariam Ulega akibonyeza kitufe kuashiria kuzinduliwa kwa taasisi wa CHAWA WA MAMA(NA SHUSHU JOEL) |
Akizindua Taasisi hiyo Mariam Ulega alisema kuwa ni mengi yamefanyika katika Taifa hili lakini wanawake wengi wako kimya.
Aidha aliongeza kuwa ni Rais wetu kipenzi Mama Samia Suluhu Hassan amefungulia mikutano ya hadhara hivyo sasa ni vyema kila Chawa wa Mama ajiandae kwa hoja kwani maendeleo yanafanywa ni makubwa kwa wananchi.
" Unapokuwa CHAWA wa MAMA kazi yake ni kuwaeleza watanzania kile qmbacho Rais wetu amewafanyia watanzania katika Elimu,Afya, Miundombinu na kwenye Maji" Alisema Bi, Mariam Ulega
Mbali na hilo Mwenyekiti huyo amewakumbusha wanawake kuwajibika kama vile anavyofanywa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwashushia wananchi maendeleo.
Naye Mwajuma Mohamed kutoka Morogoro amempongeza Bi, Mariam Ulega kwa hotuba nzuri yenye kujenga umoja wa machawa Tanzania wenye lengo la kufikisha ujumbe juu ya yale yalifanywa na Rais wetu.
Aidha amemuomba Mwenyekiti huyo wa Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Pwani Bi Mariam Ulega kuendelea kuwa na moyo huyo aliounyesha kwetu machawa na kutupa nguvu ya kutembea kifua mbele kwa kusema yale yanayofanywa na Rais Samia.
MWISHO

0 Comments