Na Shushu Joel,Mkuranga
MJUMBE wa Baraza Kuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kutokea Mkoa wa Pwani Bi’ Mariam Ulega amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo amekuwa msaada mkubwa kwa wananchi kutokana na jinsi ambavyo anapambana kuhakikisha maendeleo yanawafikia Watanzania wote.

Mariam Ulega akisisitiza jambo kwenye mkutano huo(NA SHUSHU JOEL)
Akizungumza
katika Baraza la jumiuya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani alisema
kuwa Rais Samia ni nguzo kubwa kwa wanawake kutokana kuwa mstali wa mbele
katika kutatua CHANGAMOTO Ambazo zimekuwa zikiwasumbua wanawake kwa kipindi
kirefu.
“ Wanawake
nchini walikuwa na changamoto nyingi ambazo zilikuwa zikikwamisha mambo yao
mengi kutokuendelea lakini tangu Rais Samia Suluhu Hassan ashike usukani vitu
vingi vimekuwa vikienda kutokana na kupelekwa kwa fedha nyingi kwa jamii ili
kumaliza changamoto hizo” Alisema Mariam Ulega
Aidha amewataka wanawake wote nchini kuendelea kuunga mkono juhudi kubwa ambazo zinafanywa na Rais wetu kipenzi Dkt Samia Suluhu Hassan kwani utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) umekuwa ukifanyika kila kukicha na wananchi wanajionea kile walichokuwa wakikihitaji kinafanikiwa kwa wakati.
![]() |
| Baadhi ya wanawake wa jumuiya hiyo wakimsikiliza Bi, Mariam Ulega kile anachowaelekeza katika mkutano huo. |
Naye Mariam Masaninga
ambaye ni diwani wa viti maalum amempongeza mjumbe huyo kwa ushauri mkubwa
alioutoa kwa wanawake wa wilaya ya mkuranga.
Aidha
amemtaka Mariam Ulega kuendelea kutoa ushauri kwani maneno yake yamekuwa
yakijenga sana jumuiya na chama kwa ujumla.
MWISHO

0 Comments