" VIJANA NI NGUZO YA TAIFA" MWENYEKITI UWT PWANI.

 Na Shushu Joel, Pwani.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani Bi, Zaynabu Vulu akisisitiza jambo (NA SHUSHU JOEL)

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania Mkoa wa Pwani Bi Zaynabu Vulu amewaasa vijana kuweza kujitambua kuwa wao ni tegemeo kubwa katika Chama Cha Mapinduzi ( CCM) na jumuiya zake.


Rai hiyo ameitoa alipokuwa  akizungumza na wana chama wa Chama hicho katika wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani ambapo Mbunge wa Jimbo hilo alipokuwa akiwasilisha utekelezaji wa ilani wa mwaka 2022.


Vulu alisema kuwa Vijana ni tegemeo kubwa la Taifa kutokana na kuwa na nguvu,akili na uhalaka wa kufanya jambo katika masuala mbalimbali ambayo wamekuwa wakielekezwa na viongozi wao.


Aidha alisema kuwa jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) imekuwa ikiwatumia vijana hao vile ipasavyo ndio maana jumuiya hiyo inazidi kuonekana ni bora kila wakati.


" Hivyo niwakumbushe vijana kuendelea kusonga mbele na kuwapuuza wale wanaowakatisha tamaa katika kutimiza ndoto zao" Alisema Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani Vulu.


Mbali na hayo Mwenyekiti huyo amewakumbusha vijana kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na serikali yetu ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan 


Juma Mwalamani ni moja wa kijana ambaye ni mkazi wa wilaya ya Kisarawe amemsifu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzani Mkoa wa Pwani ( UWT ) kwa jinsi ambavyo ametuelezea vijana kuwa Wazalendo wa dhati  kwa Taifa letu.


Aliongeza kuwa Mama Vulu amejitofautisha na umwenyekioti wake bali ameongea kama mzazi hivyo vijana ni vyema kuzingatia mafunzo yanayotolewa na wazazi wetu.


Hivyo ni wakati wetu vijana kuweza kutambua na kuzingatia ushauri wa kipekee ambao tumekuwa tukuupata kutoka kwa wazazi na viongozi wetu na hii itatusaidia kuondokana na vishawishi  vibaya  ambavyo  ni vya aibu  kwa familia zetu na  Taifa kwa ujumla.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments