SERIKALI YASISITIZA MATUMIZI YA MBOLEA

NA SHUSHU JOEL

  

 Serikali imehimiza matumizi ya mbolea kwa wananchi wa Kijiji cha Mlali Iyegu kilichopo Kata ya Mlalikatika Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma ili kuepuka upungufu wa chakula kwa kuzalisha mazaokwa wingi kwa kutumia mbolea inayotolewa kama ruzuku kutoka Serikalini.


Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipokua akiongea na

wananchi hao wakati wa ziara yake iliyolenga kusisitiza utunzaji wa mazingira, kilimo na

kukahamasisha agenda ya elimu."Asilimia 90 ya Wakazi wa Kongwa ni wakulima na wanategemea kilimo kuendesha maisha yao.


Nawasisitiza kufanya kilimo cha kisasa kwa kutumia mbolea kwani Serikali imeamua kuwapunguzia

mzigo wa gharama kwa kuchangia asilimia 70 ya gharama hizo. Hakuna Serikali inayotaka kudhuru

watu wake, mbolea inayotolewa ni bora na imepimwa kitaalamu. Hatutarajii kupata maombi ya

chakula cha msaada kutoka Serikalini wakati uwezekano wa kutumia pembejeo bora na kupata

chakula cha kutosha upo" Amesema Mhe Senyamule.

Katika ziara hiyo pia, Mhe. Senyamule aliweza kutembelea shule mpya ya Sekondari iliyojengwa kwa

fedha za Serikali iliyopo katika Kijiji cha Ihanda, Kata ya Mlali inayotarajiwa kuanza kupokea

wanafunzi Januari 9 mwaka huu. Shule hii inatarajiwa kuwa msaada kwa wanafunzi wa Kijiji hicho

ambao walikua wakitembea umbali mrefu wa takribani kilometa 12 kila siku kwenda na kurudi.

"Nimefurahishwa na ukamilishwaji wa shule hii ambayo itaepusha watoto kutembea umbali mrefu

kufuata shule ya Sekondari Mlali. Serikali imetimiza wajibu wake hapa na wazazi mtimize wajibu

wenu wa kuhakikisha watoto wanafika hapa shuleni" Amesisitiza Mhe Senyamule

Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Remidius Mwema, amesema kuwa walipokea fedha za ujenzi wa

madarasa 70 katika Wilaya yake na yote yamekamilika hivyo watahakikisha watoto wote 7,719

wanaotarajiwa kuanza shule mwaka 2023, wanawasili shuleni. "Tumeweka jitihada za uandikishwajiwa shule za awali na msingi kwa kwa kuhimiza mabalozi na wenyeviti wa Mitaa kutembea nyumbakwa nyumba kuhakikisha kila mtoto anayestahili kwenda shule anakwenda"


Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kongwa Bw. White Zuberi amesisitiza suala la elimu kwakusema; "Tumetumia fedha za Madarasa kujenga shule mbili ikiwemo hii ya Ihanda, Mhe. Raisanawasaidia watu wa chini kuweza kusoma mpaka ngazi ya juu kwa kutoa elimu bure kuanzia awalihadi kidato cha sita, hivyo tuunge mkono juhudi za Rais kwa kupeleka watoto shule"



Kwa upande wa sekta ya mazingira, Mhe. Senyamule ameendelea kuhimiza kampeni yakealiyoizindua Desemba 31 mwaka Jana kwa kuwataka wanakongwa kupanda miti ya kutosha nakutunza vyanzo vya maji pia kuepuka ukataji miti holela. Sambamba na hilo, alionyesha mfano kwakupanda Miti kwenye eneo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo pamoja na eneo la shule ya SekondariIhanda kama ishara ya kusisitiza wananchi kupanda miti na akasisitiza Wilaya hiyo kuhakikishainafikia lengo la agizo la Serikali la kila Halmashauri kupanda miti 1,500,000 kwa mwaka.



Vilevile katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa alitembelea mradi wa ujenzi wa kituo mahiri cha nafaka kilichopo eneo la Mtanana ambacho kitakua na utaalamu wa kuzuia sumu kuvu kwenye mazao.Mradi huu upo chini ya Wizara ya Kilimo na unagharimu takribani kiasi cha Shilingi Bilioni 19."Nimepata taarifa kituo hiki ni kikubwa Afrika Mashariki na kati, kitawezesha mazao yetu kuuzikakimataifa. Nimefarijika kusikia kuwa kituo hiki kitatoa mafunzo, hivyo naamini kitatoa darasa tosha.Naahidi sisi kama Mkoa, tutaendelea kusimamia mradi huu ili ukamilike kwa wakati na uboraunaotakiwa" Amesema Mhe. Senyamule.


Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kongwa Bw. Omary Nkullo, amesema kujengwa kwa kituo hikini kutokana na historia iliyotokea miaka mitano iliyopita ambapo Mkoa ulipata vifo vya watu nawanyama kutokana na kula sumu kuvu kwenye mazao hivyo Wizara iliandaa mpango wa kutafutaeneo kwa ajili ya ujenzi na eneo hili tulihamisha wananchi kwa fidia ya Shilingi Milioni 8 hadi 9 na hatiya umiliki ikakabidhiwa Wizara ya Kilimo kwa ajili ya ujenzi wa kituo hiki.

Post a Comment

0 Comments