WAZEE WAMTAJA ULEGA KUWA NI MKOMBOZI WA MKURANGA.

 Na Shushu Joel, Mkuranaga.

Baadhi ya Wazee wakimsikiliza mbunge wa jimbo hilo alipokuwa akizungumza na wananchi(NA SHUSHU JOEL)

WAZEE wa Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani wamemtaja Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega kuwa ndiye Mbunge pekee aliyeing'arisha Mkuranga kwa Maendeleo ikilinganishwa na wote waliopita.


Wakizungunza kwenye mkutano wa utekelezaji wa ilani ndani ya mwaka mmoja uliitishwa na Mbunge wa Jimbo hilo uliofanyika katika kata ya Mkuranga Wazee hao walisema kuwa sasa Jimbo la Mkuranga limepata mwakilishi.


Abdulitalibu Tula (78) ni Moja wa Wazee wa muda mrefu katika wilaya ya Mkuranga alisema kuwa amefanikiwa kuwaona wabunge wote waliopita katika Jimbo là Mkuranga lakini Ulega ni kinara wa ufanikishaji wa maendeleo kwa asilimia kubwa kwa wananchi.


Aliongeza kuwa Mbunge  Ulega amekuwa akitumia nafasi hiyo kwa kufanya ushawishi wa hali ya juu kwa serikali ili kuleta mabadiliko katika sekta za maendeleo hapa Mkuranga.


" Tulikuwa nyuma sana kwenye sekta nyingi lakini angalau tunaona nuru yeny ekung'aa " Alisema Tula.


Naye Bi' Cellina Hamis (67)  amempongeza Mhe. Ulega kwa jinsi ambavyo amekuwa akipambana na maendeleo kwa ajili ya Wananchi wa maeneo mbalimbali kitu ambacho miaka ya nyuma ilikuwa ni historia tu na hii ni kutokana na viongozi tuliokuwa nao.

Pia alisema kuwa Wanawake tulikuwa tukitumia muda mwingi kutafuta maji katika maeneo ya visima lakini leo maji ni kila nyumba hizi zote ni juhudi za Mbunge Ulega.


" Kweli kijana amekuwa mkombozi mkubwa kwa Jimbo la Mkuranga kutokana na kile ambacho amekuwa akikitenda kwa jamii na ndio maana hata sisi Wazee tumekuwa tukimuombea heri na baraka kubwa kutoka kwa Mungu ili azidi kutuletea maendeleo mengi.


Aidha amewataka vijana wa sasa kuendelea kumuiimba Ulega kwani sie Wazee tunajua tulikotoka katika sekta ya maendeleo.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments