MWENYEKITI WA CCM MKURANGA AWANYOOSHEA KIDOLE WANAOJIPITISHA PITISHA.

 Na Shushu Joel, Mkuranga.

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani  Nudgu  Juma Magaila amewaonya wale wote wanaofanya vikao vya siri siri kwa viongozi na wanachama wa Chama hicho wenye malengo ya kutaka nafasi ya kuwa wabunge katika uchaguzi ujao wa 2025.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mkuranga akimsikiliza kwa makini mbunge alipokuwa akinena jambo na wananchi.(NA SHUSHU JOEL)

Kauli  hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na Wananchi katika mkutano Mkuu wa mwisho wa mwaka ambapo Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega alikuwa akiwasilisha utekelezaji wa ilani ndani ya mwaka mmoja kwa yale aliyoyafanya kwa wananchi.


Aliongeza kuwa ni aibu kubwa kuwaona watu kama hao wanajipitisha pitisha kwa kuwaandaa wanachama na Viongozi wa chini wa CCM kuwa watawasaidia mambo mengi huo ni uongo na wala jambo hilo wanalolifanya alikubaliki katika Chama chetu.


"Tabia za aina hii ni mbaya sana kwenye chama chetu kutokana na kanuni zetu za chama na utaratibu wake wa kuheshimu kanuni na kumuheshimu aliyeko madarakani" Alisema Mwenyekiti Magaila 


Akisema juu ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  kwa kipindi cha mwaka mmoja Mbunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongwazwa n Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali katika wilaya yetu. 


Aliongeza kuwa miradi mingi imetekelezwa ndani ya muda  mfupi hivyo kila mwananchi anatambua jinsi gani Rais Samia alivyo na uchungu wa maendeleo kwa watanzania Alisema Ulega.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments