Na Shushu Joel, Kibaha
![]() |
Katibu wa UWT wilaya ya Kibaha Vijijini Nurath Mkandawile akipanda miti kuhamasisha wananchi kuendelea na zoezi hilo.(NA SHUSHU JOEL) |
Rai hiyo ameitoa ofisini kwake alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo vya habari mbalimbali.
Mkandawile alisema kuwa kumekuwa na changamoto nyingi nchini kutokana na ukataji wa miti ovyo jambo ambalo limetusababishia kukosekana kwa uoto wa Asili pia ukosefu wa mvua ya kutosha kwa ajili ya kilimo.
Hivyo Katibu huyo wa UWT wilaya ya kibaha vijijini ameiomba jamii kupanda miti na kuitunza ili iweze kuturudishia uoto wetu wa asili kama walivyokuwa wamefanya mababu zetu.
"Babu zetu waliitunza miti ndio maana walifanikiwa mambo yao kutokana na utunzaji wa mazingira ambao uliwapa neema kubwa ya uzalishaji wa mazao kutokana na kunyesha kwa mvua nyingi kutokana na uwepo wa miti" Alisema Mkandawile
Aidha alisema kuwa mbali na kupanda miti ni wajibu wetu kila mmoja wetu kuweza kuitunza miti hiyo kwa kusudi la kuleta tija kwa jamii zetu.
Naye Nikodemas Ally amempongeza katibu hiyo kwa kutoa hamasa kwa jamii kuweza kupanda miti kwa kila mmoja ili kuweza kuondokana na joto lilipo sasa.
MWISHO
0 Comments