Na Shushu Joel,Mkuranga
MWENYEKITI wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoa wa Pwani Bi, Mariam Ulega amewakumbusha wanawake kuhakikisha wanaongeza juhudi za uwajibikaji ili waweze kujiongezea kipato ili waondokanae na umasikini.
Rai hiyio
ameitoa alipokuwa Akizungumza na kundi la wanawake katika wilaya ya Mkuranga
ambapo alisisitiza ili kuondokana na umasikini ni lazima Wanawake tuweze
kujishughulisha na kazi mbalimbali ambazo zitatuongezea kipato chetu na si kile
cha kutegemea kupewa.Bi, Mriam Ulega ambaye ni Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake Mkoa wa POwani (NA SHUSHU JOEL)
“Wanawake ni
jeshi kubwa hivyo inapotokea tunashikamana kwa pamoja ni lazima tuweze kufanya
jambo kubwa na lenye manufaa makubwa kwetu wenyewe na jamii kwa ujumla” Alisema
Mariam Ulega.
Aidha
Mwenyekiti huyo amewakumbush Wanawake kuchangamkia mikopo inayotolewa na
serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan iliyopo katika kila halmashuri hivyo
mikopo hii itatusaidia kutuinua kuuchumi.
Aidha
amewataka Wanawake kuendelea kuyasema yale yote mazuri yuanayofanywa na Rais
Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye Taifa hili.
Naye Khadija
Juma amemsifu Mwenyekiti huyo kwa jinsi ambavyo amekuwa msaada mkubwa kwa
Wanawake na jamii kwa ujumla.
MWISHO
0 Comments