Na Shushu Joel,Bagamoyo
MBUNGE wa viti maalum kutokea Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani Subira Mgalu amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuzidi kuendelea kutatua changamoto ambazo zilikuwa ni sugu kwa Wanawake hapa nchni,
MBUNGE wa viti maalum Mhe, Subira Mgalu akifurahi jambo na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo mara baada ya uzinduzi wa mradi wa Maji ( NA SHUSHU JOEL)
Akizungumza katika
uzinduzi wa mradi wa maji wa kata ya Fukayosi wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani
Mgalu alisema kuwa Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amedhamilia kwa moyo wake
wa dhati kuhakikisha wanawake wanaondokana na changamoto ya maji na badala yake
wanajikita katika uzalishaji wa uchumi.
Aliongeza
kuwa Wanawake wengi walikuwa ni wahanga wakubwa wa changamoto za ukosekanaji wa
maji hivyo muda mwingi wamekuwa wakiutumia kutafuta maji na sio kutengeneza
uchumi kitu hicho kimekuwa kikimuumiza kichwa sana Mhe. Rais ndio maana
anazitatua kero hizo kila kukicha kwa kutoa fedha za miradi ya maji.
Mgalu alisema kuwa kukamilika kwa mradi wa maji katika kata ya Fukayosi unakwenda kuokoa uchumi wa wanawake wa Bagamoyo kwani wengi waliokuwa wakikesha kutafuta maji sasa wanakwenda kuzalisha uchumi wao kwani maji yako mlangoni na wanaanza kuchota bila wasiwasi.
“Rais Dkt
Samia Suluhu Hassan ni Mwanamke ndio maana amekuwa akipambana sana na
chanagamoto hizo kutokana na kuwa hata yeye amezipitia hivyo anataka changamoto
hizo ziishe kabisa na zibaki kuwa historia katika Taifa hili” Alisema Mgalu.
Aidha
aliongeza kuwa mradi huu ni mkubwa hivyo ni jukumu letu wananchi kuulinda ili uweze
kudumu kwa kipindi kirefu.
Naye Meneja
wa Ruwasa Wilaya ya Bagamoyo James Kionaumela amesema kuwa mradi huo umegharimu
kiasi cha shilingi Milioni mia tatu hamsini (350,344,596,00) zote zikiwa ni
pesa ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.
Aliongeza
kuwa Wanawake wanahaki ya kulinga sasa juu ya Rais huyu mwenye maono makubwa
juu ya utekelezaji wa miradi ya maji kwani Rais ameamua kuwatua wanawake ndoo
kichwani kwa dhati kabisa,
MWISHO
0 Comments