MBUNGE BAGAMOYO AZIDI KUSHUSHA NEEMA KWA WANANCHI WAKE.

 Na Shushu Joel, Bagamoyo 

MBUNGE wa jimbo la Bagamoyo Mharami Mkenge akifafanua jambo mara baada ya uzinduzi wa maji 9 NA SHUSHU JOEL)

MBUNGE wa Jimbo la Bagamoyo Mkoani Pwani  Mhe. Mharami Mkenge amezidi kushusha neema kwa wananchi wake wa kata ya Fukayosi mara baada ya kuwakabidhi mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 350.


Akizungumza mara baada ya kuwakabidhi mradi huo Mbunge Mkenge alisema kuwa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imekuwa ni serikali ya vitendo zaidi na sio  ya maneno.


Aidha amewataka wananchi wa kata hiyo ya Fukayosi kuwa mabarozi maana kuna watu wamekuwa wakibeza beza kile kinachofanywa sasa Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akiwanyamazisha kwa miradi .


Aidha Mhe. Mkenge amemshukuru sana Rais kwa kuwa mtekelezaji wa vitendo na hivyo inayoosheza wazi kabisa Rais Samia Suluhu Hassan hana mpinzani kutokana na jinsi ambavyo anawafanikishia wananchi wake kile wanachokihitaji.


Aliongeza kuwa Jimbo la Bagamoyo lilikuwa na changamoto nyingi za ukosekanaji wa maji lakini mpaka sasa Bagamoyo tunauhakika wa upatikanaji wa maji kwa asilimia zaidi ya 80 hii yote ni kazi ya Rais wa awamu ya sita Dkt Samia Suluhu Hassan. 


" Niwatake kuvitunza vyanzo vyetu vya maji ili hata wajukuu wetu wakikua wajue Babu zao tulifanya kazi" Alisema Mkenge.



Meneja wa Ruwasa wilaya ya Bagamoyo James ..... amemsifu Mbunge kwa ushawishi wake Bungeni na kuwa mstali wa mbele kwenye kusambaza miradi ya maji na sasa wananchi wa Bagamoyo wanazidi kupata maji ya kutosha.


Aidha amewataka wananchi kuweza kuunganishiwa maji majumbani kwao ili waweze kutumia kwa urahisi na kuacha kwenda kuchota kwenye vituo kwani maji yakiwa nyumbani kuna faida zake.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments