BUSEGA YAPUUZA AGIZO LA RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN

 Na Shushu Joel 

WAZIRI  Mkuu  Majaliwa Kassim ameshangazwa na kitendo kilichofanywa na uongozi wa halamashauri ya wilaya ya Busega Mkoani Simiyu kupuuza agizo lililotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan. 

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa akisisitiza jambo

Akizungumza na viongozi mbalimbali wa Mkoa huo Waziri Mkuu Majaliwa amesikitishwa na jinsi ambavyo viongozi wa halmashauri wanakuwa juu kuliko Rais Dkt Samia. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan aliagiza kujengwa kwa soko la kisasa katika mji wa Lamadi ambao unakuwa kwa kasi lakini nyie mmejenga katika kata ya Nyashimo hivyo mmepuuza agizo la Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa vile nyie ni waelewa sana wa masuala ya maendeleo


"naagiza soko hilo lililoagizwa na Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan Lijengwe  mara moja pale Lamadi kwani lamadi ndio mji unaokuwa kwa kasi katika wilaya ya Busega na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla" Alisema Waziri Mkuu Majaliwa

Aidha Waziri Mkuu ameshangazwa na tabia ya viongozi wa wilaya hiyo ya Busega ya kupewa agizo la Rais na wao kwenda kukaa kwenye kikao cha kamati ya fedha kisha kujadili agizo la Rais na kubadili maamuzi ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

"Mkurugenzi mlikutana na Diwani mmoja anayejulikana kwa jina la Miknes na kukubaliana soko hilo lijengwe Nyashimo na si Lmadi kama alivyoagiza Mhe, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, mbaya zaidi hata fedha zimetolewa na Rais wetu huyo huyo na nyie ndio mnakaidi agizo lake" Alisema Waziri Mkuu Majaliwa.


Waliojadili agizo la Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ni kamati ya fedha huku wakijua kabisa agizo la Rais aliwezi kujadiliwa kupitia madiwani hivyo jambo hili lililofanywa na hawa madiwani wa Busega na Mkurugenzi ni aibu kubwa na fedhea kwa Taifa letu,


MWISHO


Post a Comment

0 Comments