Na Shushu Joel, Bagamoyo
MWENYEKITI wa jumuiya ya Umoja wa Wazazi Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Ndugu Abubakari Mlawa amewasisitiza Wazazi kutorudi nyuma katika usimamizi wa suala zima la malezi kwa watoto .
![]() |
| Mwenyekiti wa Wazazi wilaya ya Bagamoyo Abubakar Mlawa akisisitiza jambo mbele ya wazazi ( NA SHUSHU JOEL) |
Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo alisema kuwa kumekuwa na mporomoko mkubwa katika malezi ya vijana wetu katika kipindi hiki ikitofautishwa na kipindi cha wazazi wetu ambapo walishirikiana kwa pamoja kuhakikisha vijana wanakuwa katika maadili mazuri ambayo yatakuwa na manufaa makubwa kwa Taifa letu.
Aliongeza kuwa wazazi wetu walifanikiwa kutengeneza misingi ya malezi bora kwa watoto wao kutokana na wao kujiwekea umoja wao kwani kila mazazi alikuwa na mamlaka ya kuonya kila jambo baya linalofanywa na watoto kwa kuadhibu au maneno makali pasipo kujali ni mwanae wa kumzaa.
Aidha Mwenyekiti huyo amesisitiza uwepo wa umoja na mshikamano kwa wazazi ili kuweza kuwasaidia watoto wetu waweze kurudi katika mstali wa maadili ambao sie wazazi tunatamani uwe kwa vijana wetu.
" Nimekuwa nikihamasisha malezi bora kwa kila mzazi pasipo kubagua mtoto kwani hii itasaidia kurudisha maadili ya zamani ambayo yamepotea " Alisema Mwenyekiti Mlawa.
Kwa upande wake Haji Said (52) mkazi wa wilaya hiyo amempongeza Mwenyekiti huyo kwa jinsi ambayo amekuwa mstali wa mbele katika kuhamasisha malezi bora kwa watoto.
Aidha amemtaka kuendeleza elimu hiyo kwani kizazi cha sasa kina changamoto nyingi ambazo wala hazielewi na zote zinatokana na malezi mabaya.
MWISHO

0 Comments