Na Shushu Joel, Bagamoyo
MWENYEKITI wa jumuiya ya Wazazi wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Ndugu Abubakari Mlawa amewaasa wazazi kote nchini kufuatilia mienendo ya wanafunzi pindi wanapokuwa shuleni na pia wanaporudi nyumbani.
![]() |
| Mwenyekiti wa Wazazi wilaya ya Bagamoyo Abubakari Mlawa akizunguma na mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo (NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza na Mwandishi wa HABARI MPYA BLOG Mlawa alisema kuwa Wazazi wengi tumekuwa wavivu kufuatilia mienendo ya watoto wetu kwa sababu za kujifanya tuko bize na maisha.
" Ni vyema tukawa karibu na watoto wetu ili kujua kile wanachokifanya pindi wanapokuwa mashuleni na si kuwaachia walimu peke yao" Alisema Mwenyekiti Mlawa.
Aidha aliongeza kuwa kumekuwa na changamoto nyingi nchini zikijitokeza juu ya malezi kwa watoto wetu hivyo ni vyema sasa tukaongeza juhudi za uthibiti wa mambo mabaya ambayo watoto wetu wamekuwa wakifanya huko mashuleni na hata mitaani.
"Mwenyekiti wetu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Rais Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ni kiongozi ambaye amekuwa muwazi kwetu wasaidizi wake ndani ya chama kwa kusema kuwa ni vyema wananchi wakapewa elimu ya kutosha juu ya malezi bora" Alisema Mlawa
Mbali na hilo Mlawa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa jinsi ambavyo amekuwa mstali wa mbele katika kuleta maendeleo kwa wananchi ambao walikuwa nayo hamu kuyaona yakifanyika.
Naye mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Kiromo Shabani Issa amemshukuru Mwenyekiti kwa moyo wake wa kuwatembelea wanafunzi na kuwapatia maneno mazuri ya ushauri kuhusu kutambua umuhimu wa shule'
MWISHO

0 Comments