VIZIWI WAKOSHWA NA MISAADA YA MARIAM ULEGA,

Na Shushu Joel, Dar

MWENYEKITI wa Idara ya Wanawake na watoto kutokea shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania ( Shivyawata) Bi, Nasirya Ally amempongeza  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Pwani Mariam Ulega kwa kukugwa na changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu na hata kuweza kuwawezesha kwa kuwasaidia mahitaji mbalimbali.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Mkoa wa Pwani Mariam Ulega Kulia akimkabidhi zawadi mwenyekiti wa Viziwi zawadi ( NA SHUSHU JOEL)

Akizunguimza mara baada ya kukabidhiwa kwa zawadi za sale kwa wanawake ambao wanakwenda kushiriki zoezi la sherehe za wanawake dunia Mwenyeki huyo wa Shivyawata alisema kuwa Mariam Ulega amewafanya wajione wako juu kama ilivyo kwa wengine.

Aliongeza kuwa tulikuwa na changamoto kubwa na ilipelekea kuonekana kuwa ni wanyonge kutokana na ulemavu wetu lakini ujio na ugawaji wa zawadi hizi unakwenda kufungua milango ya Mariam Ulega kwani amekuwa akijitoa sana kwa wahitaji wengi hata sie kumpata ni Bahati lakini Mungu atamuongezea kwa pale alipotoa.

Aidha aliongeza kuwa kupitia Mariam Ulega tunawaomba watanzania wenzetu waweze kuiga mfano wa Mwanamke huyu ambaye kwetu ametuheshimisha sana wanawake viziwi.


Kwa upande wake Mariam Ulega Mwenyekiti wa Jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi Mkoa wa Pwani alisema kuwa kutoa ni moyo hivyo kila mtu mwenye nafasi namuomba aweze kujitolea kwa wahitaji ili nao wajisikie kama tunavyojisikia sie.

Aidha aliongeza kuwa unapowsaidia wahitaji wanajisikia vizuri sana hivyo tuendelee kuwasaidia kwa mahitaji yao kwani hata sisi ni walemavu watarajiwa maana hakuna mwenye kujua mipango ya Mungu wetu kuwa kesho utakuwa nani.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments