WANAWAKE PWANI WAAHIDI KUMCHUKULIA FOMU YA UCHAGUZI WA URAIS UJAO DKT SAMIA

Na Shushu Joel

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania( UWT) Mkoa wa Pwani Zaynabu Vulu kwa niaba ya wanawake wenzake Mkoa wa Pwani wameahidi kumchukulia fomu ya kugombea nafasi ya Urais mwanamke mwenzao ambaye pia sasa ni Rais wa jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassn ili aweze kuendelea kuwaongoza watanzania ambao mpaka sasa kuna mambo makubwa ameyafanya.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani Zaynabu Vullu akiwaonyeoshea mikono wanawake wa Mkuranga  ( NA SHUSHU JOEL)

Hayo wameyasema katika sherehe za kuelekea siku ya mwanamke dunia kiwilaya katika wilaya ya Mkuranga ambapo kiwilaya maadhimisho hayo yalifanyika kwenye wilaya hiyo.

Akitoa sababu za wao kama wanawake kuchukua fomu ili Dkt Samia suluhu Hassan ni kutokana na utendaji wake wa kazi anazozifanya katika Taifa kwani mambo makubwa ameyafanya katika nchi hii katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Afya, Elimu, Mindombinu, Maji na mengine mengi.

“Wanawake tuna jambo letu ambalo tunahitaji kulikamilika ili kuwadhihirishia wanaume kuwa sie wanawake tunaweza kwani tumeanzia kwenye utendaji wa kazi wa Rais Samia sasa nasi kama wanawake tunamwakikishia tutamwaminisha” Alisema Vulu.

Naye Fatma Mkoga amempongeza Mwenyekiti wa UWT kwa jinsi ambavyo amekuwa mstali wa mbele katika kumsemea Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa yale ambayo amekuwa akiyafanya kwa wananchi wa wote lakini pia kuwafuta machozi Wanawake kwa asilimia kubwa kitu ambacho watangulizi wake walikisahau kidogo.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments