Julieth Ngarabali. Bagamoyo.
Imeelezwa kwamba walimu wanaofundisha madarasa ya awali ,la kwanza na la pili ni watu special (kipekee) zaidi kwa sasa kwa sababu wana wajibu mkubwa wa kumuandaa mtoto katika ujifunzaji wa kusoma,kuandika na kuhesabu ( KKK)
Hayo yameelezwa na Katibu tawala Mkoani Pwani Zuwena Omar wakati akifunga mafunzo ya siku tano kwa walimu wa shule mbalimbali Mkoani humo waliokua wakijengewa uwezo wa namna ya kutengeneza zana bora na za kudumu kwa kutumia makunzi mbalimbali zitakazoweza kumsaidia mtoto kwenye elimu yake ya awali .
Zuwena amesema Serikali sasa imetambua kwamba walimu wenye uwezo mzuri wa kufundisha, badala ya kufundisha madarasa yale ya mitihani na mengine ya juu pekee sasa wafundishe madarasa ya chini yakiwemo yale ya awali ,la pili na la tatu ili kuwaandaa vizuri zaidi wakiwa huko na sio wakiwa madarasa ya juu hasa Ile ya mitihani.
" Mwalimu anayejua vizuri kingereza aanze kufundisha darasa la tatu ,akafundishe maana apo ndio mwanafunzi Sasa anaanza kutumia kingereza ,akafundishe pale badala ya kufundisha darasa la saba"amesema Zuwena na kuongeza
'niwaombe tukawashawishi na wengine maana nafahamu muda mwingine mtu akiwekwa kwenye darasa la awali, la kwanza ,la pili wengi wanakua hawajisikii vizuri wanaona kama sijui vipi, mpango wa Serikali sasa hivi tumetambua walimu wenye uwezo mzuri wa kufundisha badala ya kufu kuwajenga watoto vizuri" amesema
Zaidi ya walimu 120 wa shule tofauti kutoka halmashauri zote mkoani Pwani wamepata mafunzo hayo yaliyokua yakitolewa na wakufunzi kutoka Taasisi ya elimu Tanzania na wataalamu kutoka kwenye mradi wa shule Bora nchini
Baadhi ya walimu hao akiwemo Hilda Sitambuli wameshukuru kuongezewa ukakamavu katika ufundishaji madarasa ya awali na wameahidi utekelezaji wenye tija kwenye maeneo yao na kuahidi kuifikisha elimu waliyoipata kwa wenzao ili iwe chachu ya kumaliza changamoto ya wanafunzi wasiomudu stadi za kazi.
Naye Mwalimu Christina Kamamba katika mafunzo wameweza kujifunza namna bora ya kutengeneza zana za kufundishia zitakazoweza kumsaidia mtoto katika ujifunzaji wa masomo mbalimbali ikiwemo hesabu ,Sanaa,lugha na sayansi .
Sekta ya elimu na mafunzo kwa mujibu wa Dira ya maendeleo ya Taifa ya 2025 na mpango wa muda mrefu wa maendeleo ya Taifa 2011/12 hadi 2024/2025 inatarajiwa kuleta maendeleo ya haraka ya rasilimali watu kwa kutayarisha idadi ya kutosha ya Watanzania walioelimika na kujielimisha zaidi ili kulifanya Taifa lipate maendeleo na kuwa lenye uchumi wa kati na ushindan ifikapo mwaka 2025,
Na ili kufikia lengo hili, mfumo wa elimu na mafunzo unaotumika nchini lazima utoe fursa za kutosha kwa watu kujielimisha, ikumbukwe kuwa elimu ya awali inanzia mtoto wa miaka mitano kwa shule za Serikali na miaka mitatu Kwa shule binafsi.
Mwisho

0 Comments