Na Eleuteri Mangi-WUSM,Dodoma
![]() |
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amekutana na
kufanya mazungumzo na Naibu Balozi wa Uswisi hapa nchini ambaye pia ni Mkuu wa
Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Leo Näscher kuhusu ushirikiano
katika eneo la Utamaduni na Sanaa baina ya nchi hizo mbili.
Kikao hicho kimefanyika Machi 9, 2023 katika ofisi za Wizara hiyo yenye Makao yake
Makuu katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Bw. Yakubu ameeleza azma ya Serikali katika kusimamia sekta za
Utamaduni, Sanaa na Michezo ambazo zinatoa ajira kwa vijana wengi na zina mchango
mkubwa katika ukuaji wa uchumi nchini na namna watakavyoshirikiana katika
kubadilishana utaalam na uzoefu katika sekta hizo.
Naye Bw. Leo Näscher Naibu Balozi wa Uswisi hapa nchini ambaye pia ni Mkuu wa
Kitengo cha Ushirikiano wa Kimataifa amesema wana Jukwaa la Maendeleo ya Sekta
ya Utamaduni (DGP) ambalo linaundwa na Balozi mbalimbali ambapo kwa sasa
linaongozwa na Wenyeviti ambao ni Uholanzi na Uswisi wataendelea kushirikiana na
Wizara hiyo na watakuwa kiunganishi na wadau mbalimbali wa sekta za Utamaduni na
Sanaa wakisaidia katika nyanja za utaalam na ushauri.
0 Comments