Na Shushu Joel, Ilala.
MLEZI wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ilala wilaya ya Ilala Mkoani Dar es Salaam Ndugu Imran Jaffer mewakabidhi baiskel za miguu mitatu walevu ili ziweze kuwasaidia katika shughuli zao za kila siku.
Akizungumza
na HABARI MPYA MEDIA Imran alisema kuwa ameamua kujitolea na atazidi kuwa
wananchi mahitaji maalum ili kuweza kuendani na serikali.
Alisema kuwa
ni muhimu kujitoa kwa jamii na hasa kwa watu wenye uhitaji ili kuwawezesha nao
kujiona wanapendwa na wana jamii wenzao.
Aidha Imran aliongeza kuwa ataendelea kujitoa kwa jamii ili aweze
kuwawezesha kupata
mahitaji yao muhimu kutokana na kuwa yeye ni mtu wa jamii sana.
Kwa upande
wake mmoja wa wapokeaji wa baiskel hizo za miguu mitatu ambaye hakutaka jina
lake litajwe alisema kuwa zawadi hizo zimekuja kwa muda sahihi kutokana na
wengi wao kutokuwa na pesa za kununua baiskel hizo hivyo tutaendelea kumuombea
dua Imran ili aweze kufanikiwa Zaidi ya hapo ili aweze kujitoa Zaidi
MWISHO

0 Comments