MNEC JUMAA AWAPA SOMO ZITO UVCCM ILALA.

Na Shushu Joel, Dar.

MJUMBE wa halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Taifa kutokea wazazi ( MNEC) Hamoud Jumaa amewataka jumuiya ya Umoja wa Vijana wilaya ya Ilala  Mkoa wa Dar es Salaam (UVCCM) kuendeleza jumuiya hiyo kwa misingi mikubwa iliyowekwa na viongozi waanzilishi wa jumuyiya hiyo.

MNEC Hamoud Jumaa akiveshwa skafu na vijana wa skauti wa Ilala mara baada ya kuwasili katika viwanja vya karinjee ( NA SHUSHU JOEL)

Rai hiyo ameitoa nalipokuwa akizungumza na Vijana wa wilaya ya Ilala katika Mkutano wa Baraza la umoja huo katika viwanja vya Karinjee ambapo amewakumbusha kuwa Jumuiya hiyo iliundwa na CXCM kwa mahususi makubwa ili iweze kuwa msaada mkubwa katika chama hicho.

Aliongeza kuwa Jumuiya ya Vijana ni tanuru kubwa la kuoka viongozi kwa ajili ya kesho ndani ya Chama Cha Mapinduzi  na Serikali kwa ujumla hivyo ni vyema kila mmoja wenu kuweza kutumia ujana wake vizuri ili hapo baadae Taifa liweze kunufaika nanyi.

“Kumbukeni na mimi nilikuwa kijana hapo zamani sasa hivi mie ni mzee sasa mnapaswa kuendeleza maadili yaliyo mema kwa nchi yetu ili muwe walithi sahihi kama vile mnavyoandaliwa na wazazi wenu” Alisema Hamoud Jumaa (MNEC)

Kwa upande wake Albert Sweya ambaye ni mmoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ilala amempongeza MNEC kwa ushauri wake kwa vijana ambao wengi wao wameonekana kuwa na tamaa ya mafanikio ya haraka kitu ambacho kimekuwa kikiwakwamisha wengi wao.

Aidha amewataka vijana kutumia ushauri uliotolewa na kiongozi huyo ili kuweza kulisaidia Taifa letu hapo kesho.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments