Na Shushu Joel
![]() |
| Naibu waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete akifafanua jambo |
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais -Utumishi na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka watendaji wa Taasisi ya Uongozi kuendelea na kazi nzuri wanayoifanya huku akiwakumbusha kuweka misingi imara ya kuanzisha kwa taasisi hiyo.
Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na viongozi mbalimbali wa taaisis hiyo ambapo walikuwa katika kikao kazi kilichofanyika katika jiji la Dodoma.
Aidha Kikwete aalisema kuwa kuanzishwa kwa taasisi hiyo kutasaidia kupunguza changamoto mbalimbali zinazowakabili watumishi nchini.
Pia Naibu Waziri Kikwete alisisitiza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza utoaji wa huduma za haraka kwa wananchi.
MWISHO

0 Comments