NA DENNIS SIKONDE , SONGWE
Mkuu wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe Mhe Farida Mgomi amelipongeza shirika la umeme Tanzania (TANESCO) wilayani humo kutoa elimu Kwa wananchi juu ya matumizi ya mfumo mpya wa NIKONECT ulioanzishwa na shirika hilo nchini Ili kuondoa mrundikano wa wateja ofsini.
![]() |
Mkuu wa Wilaya ya Ileje Farida Mgomi akisisitiza jambo mbele ya watumishi wa Taanesco |
Mgomi ametoa pongezi hizo Machi 27,2023 baada ya kutembelea na kuzungumza na watumishi wa shirika hilo, baada ya kutembelea Taasisi zinginine za serikali ikiwepo TAKUKURU, Shirika la Posta, Shirika la Simu ( TTCL), POLISI , Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) kwa lengo la kujionea namna utendaji kazi unavyoendelea.
Mgomi amesema huduma ya NIKONECT imekuja wakati sahihi ambapo imepunguza foleni katika ofisi mbalimbali za shirika hilo kwani wananchi wanapata huduma wakiwa nyumbani na kuunganishiwa umeme ndani ya siku chache kutokana na uimara wa mfumo huo.
"Mmesema mfumo huu umesaidia kuongeza idadi ya wateja kwani awali mlikuwa mkiwaunganishia wateja 45 Kwa mwezi lakini baada ya kuanzishwa Kwa mfumo huo mnaunganisha wateja zaidi ya 100 hivyo endeleeni kutoa elimu sahihi kwa wananchi Ili wauelewe zaidi mfumo wa NIKONECT", amesema Mgomi.
Aidha Mgomi amesema vijiji 22 vilivyosalia kati ya vijiji 71 vilivyopo wilayani humo vinatarajiwa kuunganishiwa umeme, huku vitongoji 35 vitawekewa umeme wa ujazilizi lengo ni kuwafikia wananchi Kwa awamu kwenye vitongoji na vijiji vyote nchi nzima.
"Mpaka Sasa wilaya ya Ileje imefikiwa na umeme Kwa asilimia zaidi ya 70 hivyo jitihada za elimu Kwa wananchi kutoka Kwa viongozi wa shirika hilo kutapelekea ongezeko la usambaji wa umeme majumbani",amesema Mgomi.
Kwa upande wake kaimu meneja was shirika Hilo wilayani humo Kassian kipanga amesema kuanzishwa Kwa mfumo wa NIKONECT kumepunguza mrundikano wa wateja kutokana na elimu inayoendelea kutolewa wananchi kupata huduma Kwa njia ya mtandao na watumishi wa shirika hilo kufanya kazi kwa weledi.
"Tutaendelea kutoa elimu Kwa wananchi juu ya matumizi ya mfumo huo ambao umekuwa na mafaniko makubwa wilayani humo", amesema Kipanga.
Huduma ya NIKONECT ambayo imezinduliwa na shirika la umeme TANESCO nchini itasaidia kuhudumia wateja washirika hilo kwa haraka na kuepusha mlundikano wa watu ambao umekuwa ukitokea katika ofisi za shirika hilo.NGWE
0 Comments