Na Shushu Joel, Pwani.
MBUNGE wa viti maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Mkoa wa Pwani Bi Subira Mgalu amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ataendelea kuwa kiongozi wa Taifa letu kwa kipindi kijacho cha miaka mitano ijayo.
![]() |
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani Subira Mgalu akionyesha ishara ya miaka miato tena kwa Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan (NA SHUSHU JOEL) |
Haya alisema alipokuwa akitimiza ahadi yake ya kuwagawia Wanawake vyerehani thelasini na tano (35) wa wilaya ya Kibiti na Rufiji kwa lengo la kuwainua kiuchumi wanawake hao.
Alisema kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa kiongozi wa pekee katika Taifa hili kwa kutenda yale ambayo yalikuwa ni ndoto kwa kila Mtanzania kuona maendeleo yakuwa kwa kasi ili watanzania waweze kunufaika nayo.
" Mpaka sasa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan amefanikisha miradi mbalimbali ikiwemo miradi Afya,Elimu,Maji, Miundombinu ya barabara ikiwemo Reli ya Mwendokasi, Bwawa la umeme kuendelea na ukamilishwaji wake hii ni jambo la pekee na la ujasili kwetu Wanawake" Alisema Mgalu.
Mbunge Subira Mgalu aliongeza kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameonyesha kuwa wanawake wanapopewa nafasi ya uongozi wamekuwa wakifanikiwa kufanya maendeleo kwa asilimia kubwa sana.
Aidha Mgalu amewataka Wanawake kote nchini kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu kwani amekuwa kiongozi wa pekee sio tu nchini bali hata nje ya Bara la Afrika Rais wetu amezidi kuonyesha juhudi zake za mafanikio ya Tanzania.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Kibiti Tatu Mkumba amemwakikishia Mbunge Subira Mgalu kuwa iwe mvua iwe jua Dkt Samia Suluhu Hassan ataendelea kuwa Rais wetu kutokana na uwezo wake aliouonyesha.
Hivyo wanawake tumejipanga kumpa kura za kishindo ambazo hazijawai kutokea kwa vipindi vyote vya uongozi uliopita.
Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya utekelezaji ya UWT Mkoa wa Pwani Bi Irene lembariti amempongeza Mgalu kwa kufanikisha ahadi yake ya kuwainua wanawake kiuchumi kwa kuwapatia vyerehani ambavyo vinaenda kuwaongezea kipato
MWISHO
0 Comments