NA MWANDISHI WETU ILEJE
Katibu wa siasa na uenezi wilaya ya Ileje mkoani Songwe kupitia Chama cha mapinduzi Ndugu Maoni Mbuba ameipongeza serikali ya awamu ya sita ikiongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani kutoa fedha shilingi Bilioni 1.5 kuboresha miundombinu ya madarasa wilayani humo.
![]() |
Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Ileje akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari. |
Mbuba amesema hayo wakati akizumgumza na waandishi wa habari kuipongeza serikali na namna kama chama kitakavyosimamia fedja bilioni 1.5 zilizotolewa na serikali kupitia mradi wa boost Kwa ajili ya kujemga vyumba vya madarasa na vyoo katika shule nane za msingi.
Mbuna amesema chama cha mapinduzi wilayani humo kitahakikisha kinafuatilia fedha hizo ili kubaini kama matumizi yake yanaendana na maelekezo ya serikali.
Aidha Mbuba amesema kamati zitakazochaguliwa kusimamia ujenzi huo ngazi ya kijiji zitangulize uzalendo Kwa kuepuka na tamaa ya kuhujumu fedha ambazo zimeletwa Kwa ajili ya kutatua changamoto za uchakavu wa majengo ya madarasa.
0 Comments