MGALU AGAWA VYEREHANI ILI KUINUA UCHUMI WA WANAWAKE.

Na Shushu Joel,  Pwani

MBUNGE wa viti maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Bi Subira Mgalu amewagawia wanawake wa wilaya ya Rufiji na Kibiti vyerehanu therasini na tano (35)  kwa lengo la kuwainua kiuchumi wana mama hao

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Subira Mgalu katikati akimkabidhi mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kibiti cherehani tyari kwa kukuza uchumi (NA SHUSHU JOEL)

Akizungumza mara baada ya kuwakabidhi vyerehani hivyo Mgalu alisema kuwa Wanawake wengi wamekuwa tegemezi sana kutoka kwa wanaume wao hivyo vyerehani hivi vinakwenda kuwa chachu ya ukuzaji uchumi wa wanawake hao ndani ya jumuiya ya UWT

Walio nufaika na mgao wa Vyerehani hivyo ni wenyeviti wa kila kata na makatibu wa kila kata wa Jumuiya ya UWT pia ofisi za wilaya zimepata vyerehani vitatu ili nao waweze kusimama kiuchumi kwa kuanzisha miradi ya ushonaji.

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa akisisitiza juu ya wanawake kuweza kujisimamia katika masuala yetu ya kiuchumi ndio maana nimewapatia mitaji hii ili muweze kukuza uchumi wenu mmoja mmoja au kikundi"Alisema Subira  Mgalu.


Aidha amewakumbusha wanawake kuwa mstali wa mbele katika kukemea ukatili wa kijinsia unaoendelea kwa watoto wetu kwani Taifa letu halikuwai kuwa na mambo ya ajabu katika maadili ,hivyo kila mzazi asimamie maadili kwa mtoto wake na watoto wa mwenzie.


Mbunge huyo amewataka wanawake hao kuvitumia vyerehani hivyo ili viweze kuwainua kiuchumi na kuondokana na tegemezi ya waume wao.


Naye Mwajuma Said ambaye ni mkazi wa Rufiji amempongeza Mhe. Subira Mgalu kwa jinsi ambavyo amekuwa mstali wa mbele katika kuwapambania wanawake wa Mkoa wa Pwani.


Aidha amemwakikishia kuwa uchumi wa wanawake unakwenda kupanda kutokana na kupewa mashine hizo na sio lazima wote tuwe washinaji hata kuvikodisha inawezekana.


Kwa Upande Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kibiti Tatu Mkumba amesema kuwa Mgalu ni kiongozi mwenye maono ya mbali katika jumuiya hiyo.


Aidha amewataka Wanawake wote ndani ya Mkoa wa Pwani kuendea kumuombea kwa Mungu ili aweze kufanikiwa na kuzidi kutuletea neema zaidi


MWISHO

Post a Comment

0 Comments