"TUWAJALI WENYE MAHITAJI MAALUM" MHE. SUBIRA MGALU.

 Na Shushu Joel Kibiti.

MBUNGE wa viti maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Mkoa wa Pwani Bi Subira Mgalu amewakumbusha watanzania kuendelea kujitoa kwa moyo mmoja ili kuwasaidia watu wenye mahitaji maalum 

Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Pwani Subira Mgalu akiteta jambo na baadhi ya watu wenye mahitaji maalum mara baada ya kikao kazi ( NA SHUSHU JOEL)

Rai hiyo ameitoa alipokuwa akizungumza na watu wenye ulemavu wa wilaya ya Kibiti ambapo alisema kuwa binadamu tunategemeana hivyo kwa kila aliye na nafasi ni vyema  kujitolea kwa hali na mali ili kuwasaidia wenzatu walemavu.


Aidha Mhe. Mbunge Mgalu amewakumbusha walemavu hao kuhakikisha wanajiunga kwenye vikundi ambavyo vitawawezesha kuweza kukopesheka kupitia halmashauri zao.


Aliongeza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amekuwa kiongozi wa pekee katika Taifa hili kwani amekutana na viongozi wenu wa kitaifa na kupanga mikakati ya jinsi ambavyo nanyi mtaweza kusimama kiuchumi kama wengine.

Mhe. Subira Mgalu akiwa katika Picha ya pamoja na watu wenye ulemavu

Mbali na hayo Mbunge Mhe. Mgalu aliwapatia watu hao wenye uhitaji sadaka ili nao wakaweze kupata futari kwenye kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wilaya ya Kibiti Mwalimu Omary Mponderwa amemshukuru Mbunge Mgalu na kumtakia kila la kheri katika mambo yake ya uongozi.


Aidha Mwenyekiti huyo alisema kuwa Mgalu ni kiongozi wa pekee katika Mkoa wa Pwani na ni Tunu ya Taifa kwani Wanawake kama hawa ni wachache sana kutokea katika Mkoa huu.

MWISHO

Post a Comment

0 Comments