Na Shushu Joel, Kibaha.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani Bi, Zaynabu Vulu amewataka wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kibaha kutokufunua funua vitabu vyao kwa wanaume na badala yake wavifunike mpaka pale muda utakapofika.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani Zaynabu Vulu akigawa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule ya Wasichana Kibaha (NA SHUSHU JOEL)
Rai hiyo
ameitoa alipokuwa akizungumza na wananfunzi wa shule hiyo ambapo amewasihi
kutumia uanafuzi wai vizuri ili kutimiza ndoto zao ambazo kila mmoja amekuwa
akijiwekea katika maisha yake.
Alisema kuwa
ni vyema kila mwanafunzi kuweza kutambua thamani yake ya sasa na ndio maana
hata Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu
Hassan amekuwa akisisitiza juu ya Elimu kwa wasichana.
Aidha
Mwenyekiti huyo amewagawia wanafunzi hao Taulo za kike kwa ajili ya kutunza
mazingira ya usafi wa miili yao ili kuondoa changamoto wanazokutana nazo wakati
wa hedhi.
Pia amewakumbusha Wananfunzi hao kutambua kile kilichowapeleka shuleni hapa kwani Taifa linawategemea ili baadae waje kuwa viongozi .
“
Niwakumbushe kutambua kuwa hata sisi tulikuwa wanafunzi kama mlivyo nyie leo
hivyo ni vyema mkafunga vitabu vyenu ili baadae mje mchukue nafasi zetu hizi
tulizonazo” Alisema Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Pwani Zaynabu Vulu.
Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo Asha Juma ameupongeza uongozi wa UWT Mkoa wa Pwani kwa jinsi ambavyo umetoa elimu kwao kwa kuwakumbusha kutambua umuhimu wa kuzingatia elimu.
“ Tunawahakikishie kuwa hatutofunua vitabu vyetu na tutavitunza ili kutimiza malengo yetu ambayo yametuleta hapa shuleni” Alisema Asha.
Pia
aliongeza kuwa ni vyema kila mmoja wetu kutumia ushauri tulioupata kutoka kwa
wazazi wetu ambao wametupatia.
MWISHO


0 Comments