WATANZANIA ONDOENI SHAKA NA UTENDAJI WA RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN " MHE. JASDEEP BABHRA

 WATANZANIA wametakiwa kuondoa hofu juu ya utendaji wa kazi zinazoendelea kufanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.

Diwani wa kata ya Keko akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari

Rai hiyo imetolewa na Diwani wa kata ya Keko wilaya ya Temeke Mkoani Dar es Salaam Mhe. Jasdeep Babhra wakati  alipokuwa akikabidhi mitihani ya kujipima uwezo kwa darasa la Nne katika shule ya Msingi Magulumbasi .


Alisema kuwa Rais Dkt Samia amekuwa akitekeleza miradi ya maendeleo pasipo kukwama kwa kitu chochote kile.


 Aidha Diwani alisema kuwa   utaratibubwa kuchapisha mitihani kwa shule za Msingi kwa madarasa yenye mitihani ya kitaifa tumekuwa tukiwachapishia mitihani hiyo ili wazidi kujipabga na kujithatiti kwenye mitihani ya taifa.


" Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan ametupatia fedha nyingi sana katika miradi ya elimu na tumefanikiwa kujenga majengo mengi ya shule za msingi na sekondari kwa kusudi la watoto wetu wasome kwenye mazingira bora na salama" Alisema  Mhe. Diwani  Babhra


Mbali na hilo Diwani huyo amewakumbusha wananchi wa kata ya keko kuendelea kuwa walinzi wa miradi yote iliyokamilika ili iweze kudumu na itumike kwa kipindi kirefu.


Kwa upande wake mwalimu Mkuu wa shule hiyo John Mabeyo amempongeza Diwani wa kata hiyo kwa jinsi ambavyo amekuwa mstali wa mbele katika kuhamasisha elimu inazidi kukua katika kata hiyo.


Hivyo amemtaka kuendelea na moyo huo wa kujitoa kwa jamii. 


MWISHO

Post a Comment

0 Comments