Na Shushu Joel, Kibaha
MJUMBE wa kamati ya siasa Mkoa wa Pwani Alhaji Mussa Mansour amewakumbusha watanzania kurejea haraka kwenye vitabu vya Mwenyezi Mungu kama vinavyoelekeza juu ya maadili yaliyo mema.
![]() |
Mjumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Pwani Alhaji Mussa Mansour akisikiliza jambo kwa makini (NA SHUSHU JOEL) |
Akizungumza na waandishi wa habari wa HABARI MPYA MEDIA Alhaji Mansour alisema kuwa watu tumejisahau sana juu ya uwepo wa Mwenyezi Mungu muumba wa vyote vilivyomo na ndio maana wengi wamekuwa wakijihusisha na tabia mbaya na zisizo za kuigwa katika jamii zetu
Alisema kuwa kumekuwepo na tabia za unyanyasaji na za ukatili unaoendelea kufanyika kwa watu mbalimbali hapa nchini kitu ambacho ni cha ajabu sana katika Taifa letu lililolelewa vyema na viongozi wetu.
" Tukiwa na hofu ya Mwenyezi Mungu tutaishi kwenye misingi iliyo bora sie na kizazi chetu kutokana na watoto wetu kuiga mazuri yanayofanywa nasi" Alisema Alhaji Mansour
Aliongeza kuwa kutokana na wimbi la ongezeko la mitandao ya kijamii duniani vijana wengi wamekuwa wakiitumia vibaya lakini kuanzishwa kwa mitandao hiyo si hivyo bali ni ukuaji wa Teknolojia hivyo ni vyema tukaitumia vizuri ili iweze kutunufaisha kwa kukuza uchumi wetu binafsi huku tukizidi kuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu.
Audha Alhaji Mansour amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kusisitiza malezi mema na bora yanaendelea kwa watoto wetu ili Taifa lije kuwa na mwendelezo wa viongozi wenye hekima.
Kwa upande wake Asha Said amesifu hotuba ya Alhaji Mansour kwani imejaa mafunzo yaliyo mema .
Aidha amewataka vijana wenzake kuendelea kusikiliza wazazi kwa yale mazuri wanayoyasema juu yetu kwani asiyesikia la mkuu kuvunjika guu ni misemo iliyotumiwa na wazazi wetu.
MWISHO
0 Comments